Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TBS Yatoa Elimu kwa Waagizaji wa Bidhaa na Mawakala wa Forodha

 

                             Na Mwandishi Wetu

WAAGIZAJI wa bidhaa na mawakala wa forodha nchini, wamepatiwa elimu
kuhusiana na taratibu za uingizaji wa bidhaa nchini pamoja na usajili
wa maghala ya kuhifadhi bidhaa za chakula na vipodozi.

Maeneo mengine ambayo wamepatia elimu ni kuhusu taratibu za kufanya
maombi kwa njia ya mtandao (OAS) pamoja na kujadili changamoto
zinazoikabili sekta hiyo, hususan kwenye masuala ya viwango na mifumo
ya udhibiti ubora.

Wadau hao walipatiwa elimu hiyo jijini Dar es Salaam jana kupitia
semina waliyoandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Akifungua semina hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Yusuf
Ngenya, Mkurugenzi Upimaji na Ugezi wa shirika hilo, Johannes Maganga,
alisema semina hiyo imewashirikisha washiriki mbalimbali ikiwemo wa
kutoka Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) na Baraza la
Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA).

Wengine ni wawakilishi kutoka Shirikisho la Wakala wa Meli Tanzania
(TASAC), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Jumuiya ya Wafanyabiashara
Tanzania (JWT), Chama cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) na
wadau wengine.

Alisema lengo la elimu hiyo ni kuwawezesha wafanyabiashara kufanya
biashara zenye tija kwa taifa bila kuathiri taratibu na sheria za
nchi. Kutokana na umuhimu huo, alisema ndiyo maana semina hiyo
imewalenga waagizaji wa bidhaa mbalimbali na mawakala wa forodha
nchini.

Maganga alisema, ili kutimiza majukumu ya shirika hilo ni muhimu kwa
umma wa Watanzania kwenda sambamba na mikakati mingine ya kitaifa.
Alifafanua kwamba shirika hilo limeendelea kutoa semina kama hizo kwa
waagizaji wa bidhaa mbalimbali zitokazo nje na mawakala wa forodha
katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Tanga.

“Lakini tumepanga kufanya semina kama hii katika Mkoa wa Mbeya hivi
karibuni,” alisema. Alifafanua kwamba kwa kuzingatia kifungu cha 36
cha sheria ya viwango Na: 2 ya mwaka 2009, Serikali ilipitisha kanuni
ya udhibiti wa shehena kupitia notisi ya Serikali Na: 405 ya Desemba
25, 2009.

Alisema kanuni hizo ziliipa TBS mamlaka ya kudhibiti ubora wa bidhaa
zinazoingia nchini kabla ya kusambazwa kwenye soko la ndani.

Kwa mujibu wa Maganga, Februari Mosi 2012 ndipo shirika lilianzisha
mfumo wa ukaguzi wa bidhaa kabla ya kusafirishwa kuja nchini (PVoC)
kama mpango wa kudhibiti ubora wa bidhaa katika nchi zinakotoka, ambao
unasaidia kutatua changamoto zinazokuwepo wakati bidhaa zinapokuwa
zinakaguliwa baada ya kufika nchini.

Alitaja changamoto hizo kuwa ni mabadiliko ya mifumo ya uondoshaji wa
shehena bandarini kwa kutumia mfumo wa kielektroni, hasara ambazo
wafanyabiashara walikuwa wanapata kutokana na kuharibiwa kwa bidhaa
zinazopatikana kutokidhi viwango, hasara kwa Serikali kupitia matumizi
ya fedha za kigeni katika kuagiza bidhaa hizo na athari kwa mazingira
wakati wa uteketezaji wa bidhaa zilizofeli vipimo.

Akitoa mada kwenye semina hiyo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa
Bidhaa baada ya kuwasili nchini, Athuman Kissumo aliwaeleza washiriki
kuhusiana na faida za uamuzi wa Serikali kurejesha TBS majukumu
yaliyokuwa yakisimamiwa na iliyokuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa
Tanzania (TFDA).

Hiyo ni kutokana na mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2019 ambayo
yameleta mabadiliko katika sheria ya viwango Na: 2 ya mwaka 2009,
ambapo majukumu ya kudhibiti ubora na usalama wa chakula na vipodozi
yanafanywa na shirika hilo.

Alitaja huduma zinazotolewa na shirika hilo kwa sasa kuwa ni usajili
wa jengo, kusimamia masuala ya usalama na ubora wa chakula na
vipondozi na upimaji wa bidhaa za vyakula na vipodozi kwa lengo la
kudhibiti ubora.

Majukumu mengine ni utoaji wa leseni au cheti cha TBS kwa bidhaa za
chakula na vipodozi na usajili wa bidhaa za vyakula na vipodozi
vinavyotoka nje ya nchi.

 

8 thoughts on “TBS Yatoa Elimu kwa Waagizaji wa Bidhaa na Mawakala wa Forodha

 • October 26, 2020 at 11:46 am
  Permalink

  Where’s the postbox? is naproxen prescription only uk When they used a scale that included both traditional and alternative symptoms, there was little difference between the two groups: about 33 percent of women met the criteria for depression, compared to about 31 percent of men.

  Reply
 • October 26, 2020 at 12:26 pm
  Permalink

  this is be cool 8) hdhealthchallenge Scores, sometimes hundreds, of people die each year in ferry accidents in the Philippines, which has a notoriously poor record for maritime safety. An archipelago of 7,100 islands, ferries are the most common form of transportation.

  Reply
 • October 27, 2020 at 4:04 am
  Permalink

  We used to work together price of amitriptyline 25mg The memo went on: “He [Blair] could express satisfaction at the progress made in talks between the US and Libya to reach a Govt to Govt solution to all the legal/compensation issues outstanding from the 1980s. It would be good to get these issues resolved, and move on. The right framework is being created. HMG is not involved in the talks, although some British citizens might be affected by them (Lockerbie, plus some UK Northern Irish litigants going to US courts seeking compensation from Libya for IRA terrorist acts funded/fuelled by Libya).”

  Reply
 • October 27, 2020 at 4:46 am
  Permalink

  I’m on holiday ciprofloxacino wiki BDFM Publishers (Pty) Ltd disclaims all liability for any loss, damage, injury or expense however caused, arising from the use of or reliance upon, in any manner, the information provided through this service and does not warrant the truth, accuracy or completeness of the information provided.

  Reply
 • October 27, 2020 at 7:33 am
  Permalink

  An envelope san estrodex side effects Route initially took us through many villages, including Salford Priors, where there were vast fields of runner beans, all in “wigwam” bamboo frames. Apparently the firm supplies major supermarkets with produce. Stratford-upon-Avon seemed to have many of the three million tourists it has each year! There were no public conveniences near our bus stop, so we used the toilets in an adjacent bookmakers, we didn’t place bets on the way!

  Reply

Leave a Reply to Benito Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama