Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TBS Yateketeza Bidhaa Zisizokidhi Ubora Zenye Thamani ya Milioni 40

Na Eliud Rwechungura

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza bidhaa zisizokidhi ubora wa viwango zenye thamani ya shilingi milioni 40 ambazo ziliondolewa sokoni na Wakaguzi wa TBS kanda ya kati kuanzia mwezi Novemba, 2020 hadi Januari 15, 2021.

Zoezi hilo la uteketezaji bidhaa hizo limefanyika katika dampo Chidachi – Dodoma, leo Januari 27, 2021

Bidhaa zilizoharibiwa ni pamoja na vipodozi vyenye viambata sumu, vyakula na vinywaji ambavyo muda wake wa matumizi umepita (Expired produducts) vilivyopatikana katika maduka mbalimbali yaliyopo katika Mikoa ya Dodoma, Tabora na Singida.

Sheria ya Viwango Na. 2 ya mwaka 2009 pamoja na Sheria ya Fedha Na.8 ya mwaka 2019 mbali na majukumu mengine zimelipa mamlaka Shirika kuondoa bidhaa hafifu sokoni na kuziharibu ama kuzirudisha zinakotoka pindi zinapobainika kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.

2 thoughts on “TBS Yateketeza Bidhaa Zisizokidhi Ubora Zenye Thamani ya Milioni 40

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama