Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Tanzania Yatumia Maonesho ya KOTFA 2022 Kuonyesha Filamu ya Royal Tour kwa Wadau wa Utalii wa Nchi ya Korea Kusini

Bodi ya Utalii Tanzania kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini imetumia maonesho ya Seoul International Tourism Expo (KOTFA 2022) kuonesha Makala ya The Royal Tour Tanzania kwa Mawakala wa utalii pamoja na Waandishi wa Habari za utalii katika soko ya utalii nchi hiyo. Maonesho yameanza tarehe 23 – 26, 2022.

“Nashukuru leo tumefanikiwa kukutana na wadau wa utalii wa hapa Korea Kusini, huu ni mwanzo mzuri na tutaendelea na utaratibu huu ili wadau waweze kuvijua zaidi vivutio vya utalii vya Tanzania. Baada ya kuona filamu ya The Royal Tour, TANZANIA, wamependa kujua fursa za uwekezaji zilizopo Tanzani, jambo ambalo linaleta matumaini kwa Mawakala wa utalii wa nchi hii kuanza kuuza utalii wa Tanzania.

Hayo yamesemwa na  Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Balozi Togolani Edriss Mavura wakati wa mkutano  uliofanyika Juni 24, 2022 katika hotel ya Intercontinental Seoul Pama iliyopo  katika mji wa Seoul.

Naye Afisa Habari na Uhusiano wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi.  Augustina Makoye ametumia mkutano huo kuwakaribisha wawekezaji kutoka Korea Kusini kwani Tanzania bado ina fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii hasa kwa upande wa Malazi, Migahawa na huduma nyingine, ili iwe chachu ya kuwavutia watalii wengi kutoka katika soko la utalii la Korea.

242 thoughts on “Tanzania Yatumia Maonesho ya KOTFA 2022 Kuonyesha Filamu ya Royal Tour kwa Wadau wa Utalii wa Nchi ya Korea Kusini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama