Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Tanzania Yaendelea Kuaminiwa Kimataifa

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na waandishi wa habari, leo Machi 15, 2020 Jijini Dodoma

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO 

Tanzania imeendelea kuaminiwa kimataifa kufuatia jitihada mbalimbali inayofanya kwa ajili ya kupiga vita vitendo vya rushwa pamoja kuwekeza katika miradi mbalimbali inayolenga na kuboresha maisha ya wananchi, pamoja na kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dodoma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alisema kuwa Machi 5, 2020 Shirika la Fedha Fedha Duniani (IMF) lilikamilisha taarifa yake ya tathmini kuhusu uchumi wa Tanzania.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (kushoto), akisaini Mikataba mitano yenye thamani ya Dola za Marekani 495.59 na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru (kulia) katika hafla iliyofanyika Benki Kuu Jijini Dar es Salaam.

“Katika taarifa hiyo IMF imesisitiza kuwa Uchumi wa Tanzania uko imara na wamefurahishwa na akiba ya kutosha ya fedha za kigeni, mfumuko wa bei kuwa chini ya asilimia 5, mauzo ya bidhaa nje ya nchi kuongezeka, kuongezeka kwa kasi ya mabenki kutoa mikopo kwa sekta binafsi na kuwa na deni la taifa ni himilivu” alisema Dkt. Abbasi

“Katika kuonesha Tanzania inaaminika kimataifa, hivi karibuni tumesaini mikataba mitano na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), inayohusu utekelezaji wa miradi mitatu ya kimkakati kwa mkopo wa masharti nafuu ya Dola za Marekani milioni 495.59 ambayo ni sawa na TZS trilioni 1.14.” alisititiza Dkt. Abbasi

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (kushoto), akibadilishana nakala ya Mkataba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), Alex Mubiru (kulia) katika hafla iliyofanyika Benki Kuu Jijini Dar es Salaam, Tanzania na AfDB zimesaini mikataba mitano yenye thamani ya Dola za Marekani 495.59.

Aidha, alifafanua kuwa fedha hizo zitawezesha kutekeleza ujenzi wa miradi ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato Jijini Dodoma kwa gharama ya dola za marekani milioni 271.63, ujenzi wa barabara ya Bagamoyo – Horohoro – Lungalunga – Malindi kwa kiwango cha lami yenye urefu wa km 120. 8 kwa gharama ya dola za marekani milioni 168.76 na dola milioni 55.2 kwa ajili ya Programu ya utawala bora na kuendeleza sekta binafsi.

 

2 thoughts on “Tanzania Yaendelea Kuaminiwa Kimataifa

 • June 22, 2021 at 2:25 am
  Permalink

  671241 819655This really is great content. Youve loaded this with useful, informative content material that any reader can realize. I enjoy reading articles that are so quite well-written. 55430

  Reply
 • July 16, 2021 at 7:23 am
  Permalink

  394181 78723I discovered your weblog web site internet site on google and appearance some of your early posts. Preserve up the excellent operate. I just extra increase Feed to my MSN News Reader. Searching for toward reading far more by you later on! 903661

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama