Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Tanzania Yachaguliwa katika Baraza Kuu la ITU 2023 – 2026

Na Innocent Mungy, Bucharest

Tanzania imechaguliwa miongoni mwa nchi 48 kati ya nchi 193 wanachama wa ITU kuwa katika Baraza la Shirika la Mawasiliano duniani – International Telecommunication Union (ITU) kwa mwaka 2023 hadi 2026. Tanzania ni miongoni mwa nchi 13 zinazowakilisha Bara la Afrika.

Baraza la ITU ni chombo cha Shirika la Mawasiliano Duniani chenye mamlaka ya kusimamia masuala ya kisera ya mawasiliano ya simu ili kuhakikisha kuwa shughuli za ITU, sera na mikakati inasimamiwa kikamilifu kwa kuzingatia mazingira ya mawasiliano leo yanayobadilika kwa kasi.

Mheshimiwa Nape Nnauye (Mbunge), Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Tanzania amethibitisha dhamira ya Tanzania katika ITU kwa miaka 4 itakayokuwa katika Baraza hilo.

“Napenda kusisitiza kuwa Tanzania imedhamiria kushirikiana na nchi nyingine wanachama, Sekretarieti ya ITU na ofisi za Kanda ili kuifanya ITU kuwa chombo muhimu cha kimataifa ambacho kina mchango mkubwa katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi zote wanachama kama mjumbe wa Baraza la ITU” alisema Mhe. Nnauye.

Baada ya kumchagua Doreen Bogdan-Martin (Marekani) kuwa Katibu Mkuu wa ITU, na Tomas Lamanauskas (Lithuania) Naibu Katibu Mkuu na Wakurugenzi 3 wanaosimamia maeneo matatu ya msingi ya kazi za ITU, nchi wanachama wa Shirika hilo  la ITU wamekamilisha uchaguzi wa Baraza Kuu la ITU na Bodi ya Kanuni za Redio.

56 thoughts on “Tanzania Yachaguliwa katika Baraza Kuu la ITU 2023 – 2026

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama