Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Tanzania Tunao Uwezo Mkubwa wa Kuzalisha Mifuko Mbadala – Makamba

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba akielezea mbele ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika kikao chao leo Jijini Dodoma. Waziri Makamba alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya viongozi wakati wa utekelezaji wa Operesheni ya Marufuku ya Matumizi ya Mifuko ya Plastiki nchini inayotarajiwa kuanza tarehe 1/6/2019.

Na: Mwandishi Wetu

Tanzania inao uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko mbadala ambayo itatosheleza kufanikisha azma yake ya kupiga marufuku biashara na matumizi ya mifuko ya plastiki.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, mhe. Januari Makamba wakati akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa leo Jijini Dodoma.

Makamba amesema kuwa ni jambo la kushangaza kuona asilimia 100 ya mifuko ya karatasi inayotumika nchini Rwanda na asilimia hamsini nchini Kenya inazalishwa Tanzania huku Tanzania ikitumia zaidi ya asilimia 80 ya mifuko ya plastiki inayozalishwa nje ya nchi jambo linalokinzana na dhana ya kukuza uchumi wa viwanda.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba akielezea mbele ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika kikao chao leo Jijini Dodoma. Waziri Makamba alisisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya viongozi wakati wa utekelezaji wa Operesheni ya Marufuku ya Matumizi ya Mifuko ya Plastiki nchini inayotarajiwa kuanza tarehe 1/6/2019.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikako baina yake na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika kikao chao leo Jijini Dodoma.

“ Tunao uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko mbadala, wazalishaji wa mifuko hiyo wameithibitishia Serikali kuwa wanao uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko hiyo ambapo Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi kimesema kitaongeza uzarishaji zaidi ya maratatu huku wawezkezaji zaidi ya 50 wakiwa wameagiza mashine za kuzalishia mifuko hiyo,”Alisema Waziri Makamba.

Makamba aliongeza kuwa nchi ya Tanzania inaweza kufanikiwa katika zoezi hili kwa kuwa inazalisha mifuko mbadala ya karatasi ambayo hutumiwa kwa kiasi kikubwa na nchi jirani za  Rwanda huku kenya wakitumia asilimia kubwa ya mifuko kutoka Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi cha hapa nchini, Kenya ikitumia asilimia 50, jambo linalotoa tafsiri kuwa tunaouwezo wa kuzalisha mifuko mbadala  itakayotosheleza,” Alisema Januari Makamba.

Waziri Makamba amesema kuwa wazalishaji wa mifuko mbadala wameithibitishia Serikali kuwa wanao uwezo mkubwa wa kuzalisha mifuko hiyo ambapo Kiwanda cha Karatasi Mufindi kitaongeza uzalishaji zaidi ya mara tatu kinavyozalisha sasa huku wawekezaji zaidi ya 50 wakiwa wameagiza mashine kwa ajili ya kuzalishia mifuko hiyo.

Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba(hayupo pichani) alipokuwa akiwaeleza kuhusu utekelezaji wa Operesheni ya Marufuku ya Matumizi ya Mifuko ya Plastiki nchini inayotarajiwa kuanza tarehe 1/6/2019.

Baadhi ya Watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwaeleza kuhusu utekelezaji wa Operesheni ya Marufuku ya Matumizi ya Mifuko ya Plastiki nchini inayotarajiwa kuanza tarehe 1/6/2019. (Na: Ofisi ya Makamu wa Rais)

Katika hatua nyingine Waziri Makamba alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa kushirikiana kwa karibu na mamlaka zingine zitakazo husika katika zoezi la kutokomeza biashara na matumizi ya bidhaa za Plastiki zilizopigwa marufuku.

Akizungumzia marufuku hiyo Makamba amesema kuwa katika awamu ya kwanza marufuku hiyo inahusisha mifuko ya plastiki tu huku bidhaa zingine zinazotumia plastiki vifungashio vya plastiki kuendelea kutumika wakati utaratibu ukiendelea. Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni bidhaa za chakula, kilimo na dawa.

Utekelezaji wa katazo hilo la matumizi ya bidhaa za plastiki nchini linafuatia utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyotoa tarehe 26, April, 2019 katika maadhimisho ya Muungano jijini Dodoma.

167 thoughts on “Tanzania Tunao Uwezo Mkubwa wa Kuzalisha Mifuko Mbadala – Makamba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama