Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TANGAZO

 

 

TANGAZO KWA WADAIWA SUGU WA MADENI YA PROGRAMU YA “COMMODITY IMPORT SUPPORT (CIS) NAFOOD AID COUNTERPART FUND (FACF)”

Wizara ya Fedha na Mipango inawataka wadaiwa sugu wa madeni ya Commodity Import Suport (CIS)na FACF, walipe madeni yao mara moja. Madeni haya ni mkopo wenye masharti nafuu yaliyotolewa kwa Taasisi, Kampuni, Viwanda na Wafanyabiashara,  ambapo wakopaji walitakiwa kulipa deni bila kutozwa riba katika kipindi cha Miezi 18 tangu walipopewa mikopo hiyo. Kwa mujibu wa sheria ya CIS (The Commodity Import Support Regulation Act, CAP 261 R. E. 2002 (s.8 (1)(b), Mkopaji akichelewa kulipa katika kipindi cha miezi 18 tangu kupatiwa mkopo, atapaswa kulipa riba ya asimilia sawa na kiwango kinachotozwa na Benki Kuu ya Tanzania inapoikopesha Serikali katika kipindi husika. Zaidi ya makampuni 980 yalikopeshwa chini ya utaratibu huu.

Serikali inatangaza kwa mara ya Mwisho kufuatia baadhi ya wadaiwa ambao wameshindwa kuitikia wito wa matangazo ya awali ya tarehe 30/12/2015 na 05/04/2018. Hatua za kisheria zitachukuliwa mara baada ya kutoka kwa tangazo hili.

ORODHA YA KWANZA YA WADAIWA SUGU WA MADENI YATOKANAYO COMMODITY IMPORT SUPPORT(CIS) NA FOOD AID COUNTERPART FUND (FACF).

 1. Yusuph Manji
 • Farm Equipment Tanzania Ltd
 • Quality Group Ltd
 • Dunhill Motors Ltd
 • Quality Seed Ltd
 • Quality Garage Ltd
 1. Mohamed Dewji
 • 21st Century Textiles Ltd
 • Afritex Ltd
 1. S. S Rashid
 • Pwani Tours and Safari Ltd
 • Pwani Investment Ltd
 1. Issack Bugali
 • Dar es Salaam International School Trust Fund
 • Upoloto Farm Ltd
 1. K.B Medicare Ltd (Prof. Bernard Kirei)

7.Siza Cold Storage Co.Ltd (Stephen Wasira)

 1. Sorority Co. Ltd (Martha Lyimo)
 2. 21st Century, Afritex Ltd,
 3. Kichonge Miller (Bokeye Kangoye)
 4. Rela Investment Company Ltd (Ahiya E. Lukumayi)
 5. Bahari Motor Co Ltd (Hashim Rungwe)
 6. Andrew Traders Co Ltd (Andrew Richard Kisenge)
 7. Oth Investment Co Ltd (Boniventure Boniventure)
 8. Kiomboi Kisiriri Pharmacy Ltd (Dkt Kingu)

 

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Kikosi Kazi, Wizara ya Fedha na Mipango, Dar es Salaam, chumba Na. 352, Simu Na. +255 739403025/ 2122282285

 

KATIBU MKUU

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO


FacebooktwittermailFacebooktwittermail