Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Kiwanda cha Kuunga Trekta Mkombozi wa Wakulima Wadogo

                                                                                  Na: Lilian Lundo – MAELEZO

Kiwanda cha Kuunganisha Trekta aina ya URSUS kilichopo mkoani Pwani kimekuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima wadogo kutokana na masharti yake nafuu ya ukopeshaji wa trekta hizo.

Kutokana na masharti hayo nafuu idadi ya wakulima wadogo waodogo wanaomiliki trekta hizo kwa matumizi mbalimbali ya shughuli za kilimo imeongezeka maradufu. Read more

Serikali Yaamua Kuinua Zao la Kahawa Nchini

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

DODOMA

Serikali imeamua kuanzisha minada ya kahawa kwenye maeneo ya uzalishaji kuanzia msimu wa 2019/2020 ili kuinua zao hilo la kimkakati nchini.

Hayo yamesemwa leo Bungeni Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo,  Omary Mgumba wakati akijibu swali Mhe. Bernadeta Mushashu kuhusu mpango wa Serikali wa kuinua zao la kahawa Mkoani Kagera ikiwemo kupandisha bei ili kumnufaisha mkulima.

Mgumba amesema kuwa lengo la utaratibu huo ni kuharakisha malipo na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa minada na kuwashirikisha wakulima wengi zaidi katika mikoa inayozalisha kahawa ikiwemo Mkoa wa Kagera.

Aidha, amesema kuwa katika kuboresha mazingira ya biashara ya zao hilo, Serikali inadhibiti makato yasiyo ya tija kwa wakulima yanayokatwa kwenye Vyama Vikuu vya Ushirika na Vyama vya Msingi ili kubaki na makato yanayolenga kuendeleza zao la kahawa.

Read more