Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Taarifa kwa Umma.

 KUAHIRISHA KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa  kuwatangazia Vyama vya Siasa na umma kwa ujumla kuwa kikao na Semina ya  Baraza la vyama vya Siasa vilivyokuwa  vifanyike  siku ya  tarehe 21 na 22 Desemba 2017, Jijini Dar es salaam vimeahirishwa hadi hapo tarehe nyingine itakapopangwa.

Kikao hicho kimehirishwa kwa ajili ya kutoa fursa kwa Vyama vya Siasa na wadau wa Vyama vya Siasa  kushiriki katika  shughuli za  uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika 13 January 2018.  Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza  kutokana na mabadiliko hayo.

Jacqueline Kilama

Kny. MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

19 Disemba, 2017

81 thoughts on “Taarifa kwa Umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama