Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Taarifa kwa Madaktari Nchini

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha watanzania kuwa kwa kushirikiana na Shirika la Misaada la Al-Balsam la nchini Saudi Arabia itakuwa na kambi maalum ya matibabu ya kusaidia wagonjwa wa moyo ambao mishipa yao ya damu haipitishi damu vizuri na inahitaji kuzibuliwa kwa kuwekewa kifaa kiitwacho Stent.

Taasisi inawaomba madaktari wote wa Hospitali za Rufaa nchini kuwaleta wagonjwa wenye matatizo hayo ili waweze kufanyiwa matibabu. Wagonjwa wafike Taasisi ya Moyo  Jakaya Kikwete tarehe 26/09/2018 kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu ambayo yataanza tarehe 29/09/2018 hadi tarehe 05/10/2018.

Kwa mawasiliano zaidi piga namba zifuatazo: 022-2151379,0782-042019,0713-236502,0713-607183,0754-870969 na 0788-465169 ili uelekezwe  utaratibu wa kuwatuma  wagonjwa hao.

 Imetolewa na:

 Kitengo cha Uhusiano

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

19/09/2018

 


FacebooktwittermailFacebooktwittermail