Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

TAA Wasisitizwa Kutoa Huduma Bora

 “Niwapongeze kwa usimamizi mzuri wa viwanja vya ndege nchini na niwaagize kuwa lazima mfanye vikao vya mara kwa mara na wadau wanaofanya kazi katika viwanja hivi, ili kupunguza malalamiko na kulaumiana hasa zinapotokea changamoto za usafirishaji wa nyara za Serikali”, amesisitiza Naibu Waziri Atupele.

Naibu Waziri Mwakibete ameitaka TAA kuandaa mikakati inayotekelezeka ya kuvifanya viwanja vingine vya mikoani kujiendesha vyenyewe badala ya kutegemea fedha zinazopatikana katika Kiwanja cha Kimataifa cha Julius Nyerere cha Dar es Salaam.

“Tuna viwanja zaidi ya 50, lakini sehemu kubwa ya viwanja hivyo vinaitegemea kifedha kiwanja cha JNIA na sasa haiwezekani, jipangeni mje na mikakati thabiti ya kuhakikisha viwanja vikubwa vya mikoa vinajitegemea na kujiendesha”, amesisitiza Naibu Waziri Mwakibete.

Kwa upande Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Hamis Amiri amesema kwa sasa Mamlaka inaendelea na utekelezaji miradi mikubwa ya ujenzi wa viwanja ikiwemo kiwanja cha ndege cha Msalato mkoani Dodoma ambapo ndio makao makuu ya nchi.

Naye Meneja wa Jengo la Tatu la Abiria JNIA, Mhandisi Barton Komba ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya Viwanja na kumuahidi Naibu Waziri kuwa Mamlaka itaendelea kuzingatia viwango vya usimamizi kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na Shirika la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO).

Naibu Waziri Atupele yuko mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya kutembelea, kufahamiana na kuzungumza na viongozi na watumishi waliopo katika taasisi za Sekta ya Uchukuzi na pamoja na kukagua miradi ya kisekta.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama