Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Suluhisho la Ucheleweshaji wa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Lapatikana

Na Ramadhani Kissimba,WFM – Arusha

Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango imekuja na suluhisho la tatizo lililokuwa linasababisha baadhi ya Miradi ya Maendeleo kuchelewa kutekelezwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mlolongo mrefu uliokuwepo katika hatua za awali za utekelezaji wa miradi hiyo.

Hayo yamesemwa na Kamishina wa Idara ya Mipango ya Kitaifa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt Mursali Milanzi wakati akifungua mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Miradi ya Maendeleo – National Project Management Information System (NPMIS) yanayofanyika Jijini Arusha.

Dkt. Milanzi amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na wadau wengine kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali wakati wa uratibu au utekelezaji wa miradi na programu za maendeleo changamoto ambazo zimekuwa zikipelekea kupunguza kasi ya utekelezaji na ufuatiliaji wa miradi mbalimbali nchini.  

‘’Napenda kuchukua nafasi hii kuelezea kwa ufupi baadhi ya changamoto ambazo Wizara ya Fedha na Mipango na wadau wengine wanaoratibu au kutekeleza miradi na programu za maendeleo wamekuwa wakikabiliana nazo kwa muda mrefu ikiwemo, barua za miradi mipya na inayoendelea kupokelewa bila kuwa na viambatisho muhimu vya nyaraka za miradi, baadhi ya viambatisho kuwa vikubwa na kushindwa kuingizwa kwenye majalada na upatikanaji usioridhisha na usio wa haraka wa taarifa za miradi pindi zinapohitajika’’. Alisema Dkt. Milanzi.

10 thoughts on “Suluhisho la Ucheleweshaji wa Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Lapatikana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama