Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Sima Asisitiza Ulinzi Katika Vyanzo vya Maji

Serikali imesema itahakikisha kuwa vyanzo vya maji vinavyopeleka maji Mto Rufiji havivamiwi kwa shughuli za kibinadamu ili Mradi Mkubwa wa kufua umeme katika bonde la Mto Rufiji uweze kutekelezeka.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akitoa maelekezo akiwa katika banio la banio la mfereji wa Mnazi katika Kijiji cha Warumba, Kata ya Imalilo Wilayani Mbarali baada ya kukagua changamoto za matumizi ya maji katika eneo hilo. Kutoka kulia ni Prof Esnat Chaggu Mwenyekiti wa Bodi – Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Reuben Mfune, Izumbe Msindai Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi – Hifadhi ya Taifa Ruaha na Dkt. Samuel Gwamaka Mkurugenzi Mkuu -NEM

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Sima mara baada ya kukagua maeneo yenye changamoto za kimazingira pamoja na kutafuta ufumbuzi kwenye ikolojia ya vyanzo vya maji vinavyo changia maji katika bonde la Rufiji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *