Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Sima aagiza Wachimbaji Wadogo Kusajiliwa

Na Lulu Mussa, Songwe.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Songwe Bw. Samuel Jeremia Opulukwa (wa pili kushoto) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi wa Mazingira katika Wilaya hiyo. Kulia ni Prof Esnat Chaggu Mwenyekiti wa Bodi – Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC na Dkt. Samuel Gwamaka Mkurugenzi Mkuu – NEMC.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. MussaSima ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Songwe kuwabaini, kuwasajili nakuunda vikundi vya wachimbaji wadogo wasio rasmi ili waweze kutambulikana kufaidika na mikopo midogo midogo inayotolewa na Serikali hapa nchini.

Ameyasema hayo hii leo mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Mkoawa Songwe hususan Wilaya ya Songwe na kubaini changamoto ya wachimbaji wadogo wanaoharibu mazingira kutokana na uchimbaji holela.

4 thoughts on “Sima aagiza Wachimbaji Wadogo Kusajiliwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *