Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Shirika la Posta Tanzania Lazindua Nembo Yake Mpya

Naibu Waziri wa Ujenzi, toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa akitoka katika jengo la Makao Makuu ya Posta jijini Dar es Salaam leo alipomwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika hafla ya uzinduzi wa Nembo Mpya ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) leo. Katikati ni Postamaster Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Hassan Mwang’ombe na Meneja Uhusiano wa Shirika hilo Bw. Ngowi

Naibu Waziri wa Ujenzi toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Nembo Mpya ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Postamaster Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Hassan Mwang’ombe na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo Kanali Mstaafu Dkt. Haruni Kondo.

Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Ujenzi, toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa alipomwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika hafla ya uzinduzi wa Nembo Mpya ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) leo Jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo umeenda sambamba na uzinduzi wa Magari kwa ajili ya shughuli za Shirika hilo.

Naibu Waziri wa Ujenzi toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa akipeana mkono na Kaimu Postamaster Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Hassan Mwang’ombe wakati wa hafla ya uzinduzi wa Nembo Mpya ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo Kanali Mstaafu Dkt. Haruni Kondo.

Msanii wa Muziki Mrisho Mpoto akifurahia pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Nembo mpya ya shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.

Magari mapya ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) ambayo yamezinduliwa na Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa (hayupo pichani) katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam. Magari hayo ni Mabasi (3), Lori (1) na magari madogo (5).

Naibu Waziri wa Ujenzi toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa akifurahia pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Nembo mpya ya shirika hilo leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya Bango lenye nembo mpya ya shirika hilo mara baada ya uzinduzi rasmi wa nembo hiyo leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na: Frank Shija )

48 thoughts on “Shirika la Posta Tanzania Lazindua Nembo Yake Mpya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *