Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Yazihakikishia Ushirikiano Taasisi za Dini katika Kuleta Maendeleo

Jonas Kamaleki, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akihutubia katika  Kilele cha Mkutano Mkuu wa Kanisa la Tanzania
Assemblies of God (TAG) jijini Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia viongozi wa dini kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao katika shughuli za maendeleo nchini.

Ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akihutubia Mkutano Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) unaofikia kilele chake leo.

”Dini zina mchango mkubwa kwenye ustawi na maendeleo ya nchi kutokana na namna zinavyoshirikiana na Serikali katika kuwahudumia wananchi kimwili hasa katika masuala ya kijamii”, alisema Rais Magufuli.

2 thoughts on “Serikali Yazihakikishia Ushirikiano Taasisi za Dini katika Kuleta Maendeleo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *