Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Yatenga Bilioni 21.4 Ujenzi wa Vivuko Vipya Vitano

Na Alfred Mgweno (TEMESA)

Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) imetenga jumla ya shilingi bilioni 21.4 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vivuko vipya vitano kwa mwaka huu wa fedha 2021/2022 ambavyo vitaenda kutoa huduma katika maeneo mbalimbali ya mito, maziwa na bahari nchini.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa Ujenzi na Matengenezo ya Vivuko kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Lukombe King’ombe wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kutoka Televisheni ya Taifa (TBC) waliofanya naye mahojiano mkoani Mwanza katika kipindi maalumu cha Mulika fursa ambacho kinaangazia miradi yote ya Serikali iliyofanyika na ambayo inatarajiwa kufanywa na Serikali kwa mwaka huu wa fedha.

Mhandisi King’ombe amebainisha kuwa miradi hiyo ya ujenzi wa vivuko vipya inatarajiwa kuanza hivi karibuni na itaangazia yale maeneno ambayo yana uhitaji mkubwa zaidi wa huduma za vivuko ambayo ni Nyamisati Mafia Mkoa wa Pwani, Mwanza, Geita pamoja na Kisorya Rugezi Mkoani Mara.

Ameongeza kuwa fedha hizo pia zitatumika kwa ajili ya ukarabati wa vivuko ambavyo muda wake wa kufanyiwa ukarabati umefikia, aidha fedha hizo zitatumika kujengea miundombinu ya vivuko ikiwemo majengo ya abiria kupumzika wakati wakisubiri kivuko (Waiting lounge) ambayo yatakuwa na vyoo kwa ajili ya abiria pamoja na kutumika kwa ajili ya ujenzi wa maegesho ya vivuko.

2 thoughts on “Serikali Yatenga Bilioni 21.4 Ujenzi wa Vivuko Vipya Vitano

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama