Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Yamtoa Hofu Mkandarasi Barabara ya Mtwara – MNIVATA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akizungumza na Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Mtwara, Mhandisi Dotto Chacha wakati akikagua hatua za ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mnivata yenye urefu wa KM 50, mkoani Mtwara. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Bw. Evod Mmanda.

Serikali imemuondolea hofu mkandarasi wa kampuni ya Dott Services anayejenga barabara ya Mtwara – Mnivata yenye urefu wa kilometa 50 kwa kiwango cha lami kuwa itakamilisha malipo anayoyadai mapema zaidi ili barabara hiyo iweze kukamilika na kupitika vipindi vyote.

Ameyasema hayo Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa wakati alipokuwa akikagua mradi huo unaojengwa kwa zaidi ya shilingi Bilioni 89 na kumsisitiza mkandarasi huyo kukamilisha barabara hiyo ndani ya miezi mitatu.

“Mkandarasi endelea na kazi kwa kuzingatia viwango na ubora, maombi yenu ya madai tumeyapokea na yatafanyiwa kazi mapema”, amesisitiza Naibu Waziri huyo.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa akikagua moja ya gari la kumwaga kokoto katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Mtwara – Mnivata yenye urefu wa KM 50 inayoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami mkoani Mtwara.

Kwandikwa amesema kuwa uamuzi wa Serikali wa kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami ni mwendelezo wa mikakati ya kuboresha miundombinu hapa nchini, kwa ajili  ya kukuza shughuli za kiuchumi na za kijamii na hatimaye kuipeleka nchi katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Bw. Evod Mmanda, amesema kuwa kukamilika kwa barabara hiyo kutarahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo mbalimbali hususani katika ukanda huu wa mikoa ya kusini pamoja na nchi jirani.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa Mtwara, Mhandisi Dotto Chacha, amemueleza Naibu Waziri huyo kuwa hadi sasa mradi umefikia asilimia 75 ambapo kilometa 43 zimekamilika kuwekwa lami na kazi zilizobaki ni kumalizia kipande kilichobaki na kuweka alama za barabarani.

Pia Mkurugenzi wa Kampuni ya Dott Services, Raj Prudhvi, ameahidi kuendelea na kazi zilizobakia na kukamilisha ndani ya miezi mitatu waliyopewa na Naibu Waziri huyo.

Mradi wa ujenzi wa barabara ya Mtwara – Mnivata yenye urefu wa kilometa 50 ni sehemu ya barabara ya Mtwara – Newala – Masasi yenye jumla ya urefu wa kilometa 210  ambayo ni muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu na pia uchumi wa wananchi wa maeneo ya Nanyamba, Tandahimba, Newala hadi

33 thoughts on “Serikali Yamtoa Hofu Mkandarasi Barabara ya Mtwara – MNIVATA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *