Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Yahamisha Mnara wa Mawasiliano Kumaliza Mgogoro

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akiielekeza kampuni ya Vodacom kuhamisha mnara na ujengwe eneo la shule ili kuepusha mgogoro na mmiliki wa eneo ulipojengwa mnara huo wakati wa ziara yake kwenye mnara huo, kijiji cha Bukuku, kata ya Rufita wilayani Nyang’hwale, Geita.

Na: Prisca Ulomi, Nyang’hwale, Geita

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye ameielekeza kampuni ya simu ya Vodacom kuhamisha mnara wake uliopo kijijii cha Bukuku, Kata ya Kafita wilayani Nyang’hwale mkoani Geita ili kumaliza mgororo uliopo baina ya Serikali na mwananhi anayemiliki eneo ulipojengwa mnara huo na kuujenga kwenye eneo la shule ya Msingi kulumbai iliyopo karibu na mnara huo ili wananchi wa kata hiyo waendelee kupata za mawasiliano

Nditiye amtoa maelekezo hayo alipofika kwenye eneo la kijiji cha Bukuku ulipojengwa mnara huo wakati wa ziara yake wilayani Nyang’hwale ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwa wananchi na kupokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya hiyo,  Hamim Guyama kuwa mmiliki wa eneo hilo Bi. Rukia Kashokelo na mme wake Clement Fungameza amekataa kusaini mkataba wa Vodacom na ameridhia mnara huo ung’olewe

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye akipata maelezo ya mgogoro wa mnara kutoka kwa Mtendaji wa Kijiji cha Bukuku kilichopo kata ya Kafita, Nyang’hwale mkoani Geita, Eunice Gombanila wakati wa ziara yake kwenye eneo ulipojengwa mnara huo

Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Hamimu Guyama akitoa taarifa ya mgogoro wa mnara wa Kata ya Kafita kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) wakati wa ziara yake wilayani humo ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano. Wa kwanza kushoto ni mbunge wa jimbo hilo, Houssein Amir.

“Mnara huu kwa huyu mama uhame tu kwa kuwa upo kwenye jiwe na anataka alipwe shilingi mioni kumi kwa mwaka na anakosesha mawasiliano, amegoma kupokea shilingi milioni mbili na laki nne kwa mwaka na eneo hili kuna migodi mitatu na mapato ya takribani bilioni 20 kwa mwaka na ni eneo linalohitaji mawasiliano kwa uchumi na ulinzi na usalama wa kata ya Kafita,” amesema Guyama

Guyama amefafanua kuwa mmiliki wa eneo amefanya jitihada za kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ili kuhakikisha kuwa wanapata malipo hayo kwa kukodisha eneo lao ulipojengwa mnara na kukataa kusaini mkataba na Vodacom wa malipo ya awali waliyokubaliana

Nditiye ameipata kampuni ya simu ya Vodacom kuhakikisha kuwa inahamisha mnara huo ndani ya mwezi mmoja na amepiga marufuku kwa kampuni za simu zinazojenga minara kwa kutumia ruzuku ya Serikali wanayopewa kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kujenga mnara kwenye eneo la mtu binafsi ili kuepusha migogoro kwa kuwa Serikali haiko tayari kuingia migogoro na wananhi wake bali minara ijenge kwenye maeneo yanayomilikiwa na Serikali ya kijiji, shule au maeneo ya kanisa au misikiti ili wananchi wanufaike na fedha zinazolipwa na kampuni za simu

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Hamimu Guyama kitabu cha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote chenye orodha ya minara iliyojengwa na Serikali wilayani humo wakati wa ziara yake ya kukagua upatikanaji wa huduma za mawasiliano

Mhandisi wa Kampuni ya Vodacom, Benedict Marwa, akimshukuru Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) kwa niaba ya Serikali kwa kuielekeza kuhamisha mnara wa kata ya Kafita ili kuepusha mgogoro na mmiliki wa eneo wakati wa ziaa yake wilayani Nyang’hwale, Geita.

Naye Mtendaji wa Kijiji cha Bukuku kilichopo kata ya Rufita wilayani Nyag’hwale mkoani Geita, Eunice Gombanila ulipojengwa mnara huo amemweleza Nditiye kuwa mama huyo amekataa kupokea na kusaini mkataba baina yake na Vodacom ambapo alilazimika kukaa na mkataba huo ofisini kwake kwa muda wa wiki nne bila ya mafanikio na alipomfuata mmmiliki wa eneo hilo alikataa kusaini mkataba huo na maeridhia ung’olewe

Mkuu wa Uedeshaji wa UCSAF, Mhandisi Albert Richard amesema kuwa ujenzi wa mnara huo umegharimu dola za marekani 180,000 ambazo ni zaidi ya shiingi milioni 200 za kitanzania na kuongeza kuwa mnara huo umehujumiwa kwa kung’olewa paneli tatu za sola ambazo zinazalisha umeme wa jua kwa ajili ya kuwasha mnara huo ili uweze kuwaka na kusambaza mawasiliano kwa wananchi

Mhandisi wa Vodacom, Benedict Mara ameishukuru Serikali kwa kutoa maelekezo ya kuhamisha mnara huo na watatekeleza maelekezo hayo ili waweze kuendelea kutoa huduma za mawasiliano kwa wananchi na wakazi wa kata ya Kafita

Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kulumbai iliyopo Kata ya Kafita wilayani Nyang’hwale, James Jacob amefurahia uamuzi wa Serikali wa kujenga mnara huo kwenye eneo la shule baada ya mmiliki wa eneo ulipojengwa mnara huo hapo awali kuridhia ung’olewe kwa kutaa malipo ya Vodacom na amesema kuwa malipo hayo yataiwezesha shule kujiendesha

Mbunge wa Nyang’hwale, Houssein Nassoro Amir amemweleza Nditiye kuwa anaiomba Serikali kuboresha mawasiliano ya kata ya Nyamtukuza, Nundu, Nyijundu, Kafita, Kaboha na Shabaka kwa kuwa kuna shida ya mawasiliano na ukitaka kupata taarifa saa tano asubuhi unapata saa kumi jioni hivyo inaleta changamoto ya ulinzi na usalama

“Serikali inatumia mtandao kukusanya mapato yake ila mtu analazimika kukaa na fedha kwa muda mrefu kwa sababu usikivu wa mawasiliano sio mzuri hivyo tunashindwa kukusanya mapato ya Serikali kwa wakati,” amesisitiza Amir

Katika hatua nyingine, Nditiye amemwelekeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba na Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta kufika wilayani Nyang’hwale ndani ya mwezi huu wa Oktoba, 2019 na kufungua ofisi zao ili kuweza kuwahudumia wananchi na kusogeza karibu huduma zao

 

One thought on “Serikali Yahamisha Mnara wa Mawasiliano Kumaliza Mgogoro

  • July 17, 2021 at 7:44 pm
    Permalink

    146104 529817Youre so cool! I dont suppose Ive read anything in this way before. So nice to uncover somebody with some original ideas on this topic. realy appreciate starting this up. this excellent internet site is something that is needed more than the internet, a person if we do originality. valuable work for bringing something new towards the internet! 917329

    Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama