Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Yajipanga Uchumi wa Buluu

“Kama Serikali tumejipanga kikamilifu kupitia wataalam wanaozalishwa hapa DMI sababu Uchumi wa buluu unahitaji sana wataalm hawa katika maeneo mbalimbali hata viwandani”, amesema Naibu Waziri Mwakibete.

Naibu Waziri Mwakibete amesema ni wakati muafaka kwa wataalam kuangalia nyanja zote za uchumi huo wa buluu ikiwemo viumbe vilivyopo baharini kama miti ya mikoko, mwani na vingine ili kuwa na uwanda mpana wa namna wanavyoweza kuishauri Serikali kuanzia kwenye sera na utekelezaji.

Kwa upande wake Balozi wa Heshima wa Visiwa vya Shelisheli, Maryvonne Pool, amesema kama nchi wameweka mikakati madhubuti kuhakikisha kupitia bahari nchi inapata mapato hali inayofanya nchi hiyo kuwa na kiwanda kikubwa cha tatu duniani kinachouza samaki katika nchi za ulaya na maeneo mengine.

“Sisi tulishaanza kuitumia fursa ya uchumi wa buluu na mikakati tuliyojiwekea imeanza kuzaa matunda kwani Bahari imekuwa ikichangia sehemu kubwa ya pato la nchi yetu na kwenye hili tunalisimamia kwa karibu sababu tumeweka kanuni ambazo kwa mtu anayebainika anafanya uvuvi haramu faini ni kuanzia dola milioni moja”, amefafanua Balozi Maryvonne Pool.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya DMI, Nahodha Ernest Mihayo, ameiomba Serikali kukitazama chuo hicho kwa uzito mkubwa kwani ni chuo pekee kinachozalisha wataalam watakaoweza kutimiza lengo la Serikali katika Uchumi wa Buluu.

Mkutano huo wa kitaifa wa Uchumi wa Buluu umewakutanisha wadau mbalimbali wa usafirishaji kwa siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine utajadili na kuangalia fursa zilizopo Bahari ya Hindi na Maziwa Nchini na namna ya kuzitumia kwa manufaa ya Taifa.

37 thoughts on “Serikali Yajipanga Uchumi wa Buluu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama