Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Yaanzisha Kanda Mpya ya NFRA Songwe

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Serikali imetangaza kuanzisha Kanda mpya ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula-NFRA katika Mkoa wa Songwe itakayohudumia Mikoa ya Songwe na Mbeya.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika eneo la Vwawa mkoani Songwe jana tarehe 8 Julai 2020 Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amasema kuwa Mkoa wa Songwe ulishika nafasi ya tatu Kitaifa katika uzalishaji wa mazao ya chakula nchini katika msimu wa 2018/19 hivyo Kutokana na uzalishaji huo mkubwa wa chakula, Serikali imeona ipo haja ya kuanzisha Kanda ya NFRA katika Mkoa wa Songwe, tofauti na hapo awali ambapo katika eneo la Vwawa kulikuwa na Kituo kidogo cha NFRA ambacho kilikuwa chini ya Kanda ya NFRA Makambako.

Waziri Hasunga amesema kuwa Kanda ya NFRA Songwe imeanzishwa rasmi tarehe 01 Julai, 2020 ambapo Kuanzishwa kwa Kanda hiyo kumetokana na hali ya uzalishaji mkubwa wa chakula katika Mikoa ya Songwe na Mbeya, pamoja na kujengwa kwa Maghala na Vihenge vya Kisasa ambavyo vitaongeza uwezo wa uhifadhi kutoka tani 17,000 za awali na kufikia tani 37,000.

4 thoughts on “Serikali Yaanzisha Kanda Mpya ya NFRA Songwe

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *