Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Kuzilinda Taasisi za Kidini

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akipokea vyerehani kutoka kwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Islamic Foundation, Arif Nahdi (wapili kushoto), vilivyotolewa kwa ajili ya wananchi Visiwani Zanzibar  kuvitumia katika kujiinua kiuchumi.

Mwandishi Wetu

Serikali imesema itaendelea kuziunga mkono taasisi za kidini nchini ili ziweze kuleta maendeleo na kutekeleza majukumu yao vizuri ikiwa ni mdau muhimu katika maendeleo na ustawi wa  nchi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa kupokea msaada wa vyerehani Tisini na Nne vyenye thamani ya Shilingi Milioni Ishirini na Nne  vilivyotolewa kwa taasisi ya TAYI  inayojishughulisha na kuwaokoa vijana kutoka katika tabia hatarishi ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya.

“Serikali tumekua tukipokea misaada mbalimbali kutoka katika taasisi za kidini nchini,wamekua wakisaidia visima vya maji,mashule na kubwa zaidi wanafundisha maadili ili taifa letu liwe na watu makini wanaoweza kuliletea maendeleo siku za usoni,kwa niaba ya serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani tunaahidi kuzilinda taasisi hizi ili ziweze kufanya shughuli zake bila kubughudhiwa” alisema Masauni.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi mmoja wa wananchi cherehani zilizotolea na Taasisi ya Islamic Foundation kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi. Kulia ni  Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Arif Nahdi,

Mwenyekiti wa Taasisi iliyotoa msaada huo wa vyerehani, Aref Nahdi  amewaomba wananchi waliopokea mssada huo kwenda kuzitumia katika shughuli za ujasirimali akiamini watapata kipato zaidi endapo watazitumia vizuri.

“Nawaomba mkazitumie vizuri ili ziweze kuwaongezea kitu kwenye vipato vyenu,natoa wito msiende kuviuza kwani lengo lake ni kuwawezesha muwe na shughuli itakayowaingizia kipato na sisi kama taasisi tunaahidi kiasi cha Shilingi Milioni Moja kwa wale wanafunzi ishirini wa kwanza watakaotaka kujifunza ushonaji ili waweze kuzitumia vizuri” alisema Nahdi

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi waliopokea misaada hiyo ya vyerehani wameishukuru taasisi hiyo kwa kuwapa vyerehani hivyo huku waiwaomba wasichoke kuwasaidia mara kwa mara ili vijana wengi wawe na shughuli za kuzalisha kipato.

Baadhi ya wananchi wa visiwani Zanzibar wakiwa wamesimama mbele ya vyerehani vilivyotolewa na Taasisi ya Islamic Foundation na kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni. Kwenye hafla hiyo Naibu Waziri Masauni amezihakikishia ushirikiano taasisi zote za dini.

26 thoughts on “Serikali Kuzilinda Taasisi za Kidini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama