Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Kuwekeza Sekta ya Anga

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya (wa pili kulia), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela (kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, alipokuwa akifafanua jambo, wakati wa uzinduzi wa safari ya kwanza ya Ndege ya Shirika la Ethiopia ya kubeba mizigo ya minofu ya samaki kutokea jijini Mwanza kuelekea nchini Ubelgiji jana.

Na WUUM

Serikali imewahakikishia wafanyabiashara wa samaki jijini Mwanza kuwa itaendelea kuimarisha miundombinu na kuboresha sera ya sekta ya anga ili kurahisisha usafirishaji wa abiria na mizigo ndani na nje ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, aliposhuhudia safari ya kwanza ya Ndege ya Shirika la Ethiopia ikibeba minofu ya samaki kutokea kiwanja cha Ndege cha Mwanza ambapo aliwataka wafanyabiashara hao kuzalisha bidhaa zaidi ili kuuza mzigo mkubwa zaidi nje.

“Niwahakikishie wafanyabiashara kuwa kwa sasa jengo la kutunzia mizigo lipo na lina viwango vizuri, usafiri wa kusafirisha mizigo upo na soko lipo hivyo kazi kwenu kuchangamkia fursa hii” amesema Naibu Waziri Mhandisi Nditiye.

Naibu Waziri Nditiye, ameongeza kuwa tayari kuna maombi ya mashirika mengine ya ndege kutaka kusafirisha mizigo kupitia Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA), Dar es Salaam na Mwanza, hivyo Wizara inaendelea kupitia maombi hayo ili kuruhusu ndege nyingi zaidi kusafirisha bidhaa mbalimbali nje ya nchi.

Muonekano wa ndege aina ya Boeing Dreamliner 787-8 ya Shirika la Ndege la Ethiopia ikiwa katika kiwanja cha Ndege cha Mwanza, mara baada ya kuwasili kwa safari yake ya kwanza ya kubeba mizigo ya samaki kutokea mkoani hapo kuelekea nchini Ubelgiji.

Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya, ametanabaisha kuwa usafirishaji wa minofu ya samaki umeongeza ajira na kipato kwa wananchi wa Mwanza kwani viwanda zaidi ya kumi na tano vinazalisha minofu na kusafirisha ndani na nje ya nchi.

“Kuna ajira zimeongezeka kuanzia kwenye uvuvi wa samaki, uzalishaji wa vifungashio mpaka kwenye viwanda vinavyosindika na kupakia samaki, hivyo niwaombe wenye viwanda kuhakikisha wanazingatia viwango na masharti ili soko liweze kuongezeka ndani na nchi” amesema Naibu Waziri Mhandisi Manyanya.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewataka wafanyabishara mjini Mwanza kuwa na jukwaa la pamoja kujadili namna bora ya kuboresha bidhaa zinazolishwa na kuahidi kuwa Serikali ya mkoa iko tayari kutatua changamoto zozote watakazoziwasilisha baada ya zoezi la usafirishaji wa moja kwa moja kuanza.

Aidha, Mfanyabiashara wa samaki Edwino Oking’o amesema kuwepo kwa shirika zaidi ya moja kusafirisha mzigo wa minofu wa samaki kutachangia bidhaa hizo kuwafikia wateja kwa wakati huku mzigo ukiwa na ubora kwani kumepunguza mzunguko ambapo awali minofu hiyo ilikuwa ikisafirishwa kupitia Nairobi.

“Kabla ya safari za mashirika haya mawili la Rwanda na Ethiopia tulilazimika kuutunza mzigo mpaka ndege zipatikane au kusafirisha kupitia Nairobi, lakini sasa hivi kuna ahueni kwani mashirika haya mawili yanafanya safari zake mara mbili kwa wiki kila shirika hivyo mlaji atapata bidhaa kwa wakati na ubora” amesema Oking’o.

Shirika la ndege la Ethiopia ambalo limeanza rasmi kusafirisha mizigo ya minofu ya samaki limesafirisha zaidi ya tani 19 na limekuwa shirika la pili kuanzisha safari za mzigo kutokea Mwanza kuelekea nchini Ubelgiji, ambapo awali mizigo hiyo ilikuwa ikisafirishwa na shirika la ndege la Rwanda pekee.

 

9 thoughts on “Serikali Kuwekeza Sekta ya Anga

 • August 10, 2020 at 3:40 pm
  Permalink

  Attractive part of content. I just stumbled upon your blog and in accession capital
  to claim that I get in fact loved account your weblog
  posts. Any way I’ll be subscribing in your augment or even I success you get entry to constantly fast.

  Reply
 • August 24, 2020 at 7:32 pm
  Permalink

  I do not even know how I ended up here, but I thought this post was
  good. I do not know who you are but definitely you’re going
  to a famous blogger if you aren’t already 😉 Cheers!
  cheap flights 31muvXS

  Reply
 • August 24, 2020 at 11:38 pm
  Permalink

  Hi to every , since I am in fact keen of reading this web site’s post to be updated daily.
  It contains fastidious material. 3gqLYTc cheap flights

  Reply
 • August 26, 2020 at 5:23 pm
  Permalink

  Greate pieces. Keep posting such kind of information on your page.
  Im really impressed by your blog.
  Hello there, You have done an excellent job.
  I will certainly digg it and individually suggest to my friends.
  I am confident they’ll be benefited from this web site.

  yynxznuh cheap flights

  Reply
 • August 27, 2020 at 11:23 pm
  Permalink

  I am sure this piece of writing has touched all the internet visitors,
  its really really nice piece of writing on building up new blog.

  Reply
 • August 28, 2020 at 4:38 pm
  Permalink

  Hi there! I simply wish to offer you a big thumbs
  up for your excellent information you have got here on this
  post. I am returning to your site for more soon.

  Reply
 • September 5, 2020 at 12:38 pm
  Permalink

  Greetings! I’ve been following your site for a while now and finally got
  the bravery to go ahead and give you a shout out from Austin Texas!

  Just wanted to tell you keep up the fantastic work!

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *