Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Kuruhusu Wenye Uwezo Kuleta Mafuta

“Mpango wa kuanzisha mfuko huu uko katika hatua za mwisho za maandalizi na utakapokamilika, utawasilishwa katika Baraza la Mawaziri,” alifafanua Makamba.

Aidha, hatua nyingine ni kuanzisha Hifadhi ya Mafuta ya Kimkakati (National Strategic Petroleum Reserve), ambapo serikali inakamilisha marekebisho ya kanuni za kuanzisha na kuendesha hifadhi ya mafuta ya kimkakati ili nchi ijihakikishie usalama wa upatikanaji wa mafuta na unafuu wa bei katika vipindi kama hivi ambavyo bei ya mafuta inakuwa imepanda.

Vilevile, Serikali imechukua hatua ya kuanzisha kituo kikubwa cha mafuta (Petroleum Hub), ambapo ipo kwenye hatua ya kukamilisha makubaliano ya kujenga maghala makubwa ya kuhifadhi mafuta kwa ajili ya kuuzwa ndani na nje ya nchi kulingana na uhitaji. Uwepo wa kituo hicho utawezesha nchi kupata mafuta yenye bei nafuu pale bei zinapopanda kupita kiasi. Mpango huu na utekelezaji wake unaweza kukamilika katika kipindi cha miaka mitatu.

Hatua nyingine ni kuanzisha upokeaji wa mafuta katika ghala moja (Single Receiving Terminal – SRT) kupitia maghala ya TIPER ili kupunguza au kuondoa gharama za meli kusubiri au kuchukua muda mrefu katika upakuaji wa mafuta katika maghala mengi, ambapo gharama hizo pia zina mchango katika bei ya mafuta (dermurrage charges).

“Hatua hii itaondoa changamoto za udanganyifu na kuongeza ufanisi katika biashara ya mafuta hapa nchini. Hatua hii inaendana na kuyafanya maghala haya kuwa Customs Bonded Warehouse ili kushamirisha biashara ya mafuta yanayokuja nchini na kwenda kwenye nchi nyingine,” alifafanua Makamba.

Pia serikali inaiongezea uwezo TPDC kuagiza mafuta nje ya nchi, ambapo mara ya mwisho ilifanya shughuli hiyo miaka 20 iliyopita, pamoja na kuimarisha utendaji na weledi wa taasisi za serikali zinazoshughulika na biashara ya mafuta nchini, ikiwemo EWURA na PBPA (Wakala wa Uagizaji wa Mafuta Pwani).

Makamba amesema kuwa, hatua hizo zitafafanuliwa kwa kirefu na Wabunge watapewa fursa ya kutoa maoni na ushauri wakati wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati wiki tatu zijazo.

30 thoughts on “Serikali Kuruhusu Wenye Uwezo Kuleta Mafuta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama