Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Kuruhusu Wenye Uwezo Kuleta Mafuta

Na Lilian Lundo – MAELEZO

Serikali imesema kuwa, itaruhusu wenye uwezo wa kuleta mafuta kwa bei nafuu waweze kuleta mafuta ili kupunguza upandaji wa bei za mafuta hapa nchini.

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema hayo leo, Mei 10, 2022 bungeni Jijini Dodoma, alipokuwa akitoa kauli ya kupanda kwa bei za mafuta na hatua zinazochukuliwa na Serikali kushughulikia suala hilo.

“Wizara imekamilisha kufanya tathimini ya kampuni zote zilizoonesha nia ya kuleta mafuta kwa bei nafuu kwa lengo la kujiridhisha na uwezo wao wa kuleta mafuta hayo ili kuhakikisha uwepo wa mafuta nchini (security of supply),” alifafanua Makamba.

Aliendelea kusema kuwa, hatua hiyo ni moja ya hatua zisizo za kifedha zinazochukuliwa na serikali, mipango hii ikileta matokeo yanayotarajiwa basi bei za mafuta zitapungua zaidi kuanzia mwezi Agosti, 2022.

Makamba ametaja hatua nyingine zisizo za kifedha ambazo serikali imechukua, kuwa ni pamoja na kuanzisha mfuko wa kuhimili ukali wa bei za mafuta (Fuel Price Stabilization Fund), ambapo serikali imeandaa utaratibu wa kuanzisha mfuko maalum utakaotumika kupunguza makali ya bei ya mafuta kipindi ambacho bei hizo zinaongezeka kwa kiasi kikubwa.

32 thoughts on “Serikali Kuruhusu Wenye Uwezo Kuleta Mafuta

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama