Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Kupanga Mikakati ya Kuendeleza Sekta ya Sheria Nchini

Na Mwandishi Wetu, OWMS, Dodoma

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kuanza kupanga mikakati ya kuendeleza Sekta ya Sheria nchini kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania.

Hayo yameelezwa na Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende wakati akitoa salamu kwenye kikao kazi cha Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo vya Sheria wa kutoka Wizara mbalimbali, Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma na Halmashauri zote nchini.

Dkt. Luhende ameongeza kuwa, kikao kazi hicho kimewakusanya viongozi hao ili kupanga mikakati ya kuendeleza Sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kubadilishana uzoefu ili kupata wanasheria wabobezi ndani ya Serikali ili kuisaidia Serikali kutekeleza majukumu yake ambapo maelezo hayo yamejikita kwenye Kauli Mbiu ya Mwaka huu isemayo, “Utekelezaji wa Majukumu Unaozingatia Sheria ni Nyenzo Muhimu kwa Maendeleo ya Taifa.”

32 thoughts on “Serikali Kupanga Mikakati ya Kuendeleza Sekta ya Sheria Nchini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama