Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Kulinda Maslahi ya Wanahabari

Na Immaculate Makilika na Prisca Ulomi, Mwanza

Serikali imesema imedhamiria kulinda maslahi ya Waandishi wa Habari nchini kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye jijini Mwanza katika Uwanja wa Nyamagana wakati aliposhiriki katika tukio la kuaga miili ya Wanahabari 5 waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea jana Januari 11, 2022 katika Wilaya ya Busega mkoani Simiyu wakati wakielekea kwenye ziara ya kukagua miradi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Mhandisi Robert Gabriel.

Mhe. Nape amewataka waajiri wa waandishi wa habari waliofariki katika ajali hiyo kuwalipa maslahi yao kwa familia za marehemu.

“Natoa siku 7 kwa waajiri wote kuanzia leo kulipa haki za wanahabari waliofariki na taarifa za uthibitisho wa malipo ziwasilishwe kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza”, alisisitiza Waziri Nape

10 thoughts on “Serikali Kulinda Maslahi ya Wanahabari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama