Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Kujenga Daraja Mto Malagarasi

Serikali imesema inatarajia kujenga daraja la kudumu katika mto Malagarasi litakalounganisha kijiji cha Ilagala na Kajeje ikiwa ni mbadala wa kivuko cha Malagarasi ili kutatua changamoto ya usafiri na usafirishaji katika maeneo hayo.


Akizungumza na wananchi wa maeneo hayo wilayani Uvinza, mkoani Kigoma, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema kuwa  Serikali imeona adha wanayoipata wananchi wa hapo, hivyo imeamua ndani ya mwaka huu  wa fedha kuanza mchakato wa ujenzi wa daraja hilo.


“Sisi kama Serikali tumeona changamoto zenu hapa, hivyo tayari tumetenga kiasi cha shilingi milioni 400 ndani ya mwaka huu wa fedha 2021/2022, kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa daraja hili, baada ya kazi hii kufanyika, ujenzi utaanza mara moja, amesema Kasekenya.

Aidha, Naibu Waziri amemuagiza Kaimu Meneja wa Kivuko hicho kuhakikisha anaongeza muda wa utoaji huduma za usafirishaji unaotolewa Kivukoni hapo hususan katika kipindi cha kiangazi, kutoka  saa 12  asubuhi hadi saa 12 usiku kama ilivyokuwa awali na kusogezwa hadi saa Tatu usiku ili kuruhusu unafuu na urahisi kwa watumiaji wa huduma hiyo huku wakisubiri ujenzi wa daraja hilo kuanza.

5 thoughts on “Serikali Kujenga Daraja Mto Malagarasi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama