Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali kuendelea Kutekeleza Ahadi zake katika Kuwaletea wananchi Maendeleo-Waziri Mkuu

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hotuba yakuahirisha Bunge mapema leo Bungeni Mjini Dodoma hadi Aprili 3, 2018 ambapo amesisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kutekeleza ahadi zake katika kuwaletea wananchi Maendeleo.

Mawaziri na Wabunge wakimpongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa mara baada yakuahirisha Bunge hadi Aprili 3, 2018.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akitoa ufafanuzi kuhusu utaratibu na mfumo wa utoaji hati za Kusafiria na vibali vingine kwa kutumia mfumo wa Kielektroniki.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika akisisitiza jambo Bungeni mapema leo kabla yakuahirishwa kwa Bunge hadi Aprili 3, 2018.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasikiliza wabunge ndani ya ukumbi wa Bunge mapema leo kabla yakuliahirisha hadi April 3, 2018.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akitoka nje ya Ukumbi wa Bunge baada yakuahirishwa kwa Bunge hadi Aprili 3, 2018. (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma)


FacebooktwittermailFacebooktwittermail