Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Kuanza Utekelezaji wa Mradi Mkubwa wa Uwekezaji Dar es salaam.

Na Georgina Misama, Maelezo

Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi inatarajia kuanza kutekeleza mradi mkubwa wa uwekezaji katika eneo la Kurasini lenye ukubwa wa hekari sita lililopo wilayani Temeke Jijini Dar es salaam litakalojulikana kama Mtaa wa Viwanda na Kituo cha Biashara cha Kimataifa (Kurasini Industrial Park and Business Centre)

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya eneo hilo, Waziri wa Viwanda na Biashar,a Prof. Kitila Mkumbo alisema kuwa katika mwaka huu wa fedha  Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kuanza maandalizi ya utekelezaji wa mradi huo ambayo yanatarajiwa kukamilika Februari, 2022.

Prof. Kitila alifafanua kuwa mradi huo utahusisha mambo makubwa matano ambayo ni ujenzi wa viwanda vya kuchakata mazao ya kilimo, ujenzi wa viwanda vya kutengeneza na kuunganisha bidhaa mbalimbali ikiwemo bidhaa za umeme, ujenzi wa kituo cha kimataifa cha mazao ya kilimo na biashara, ujenzi wa maghala ya kuhifadhi mbogamboga katika hali ya uasili wa baridi na ujenzi wa kituo cha pamoja cha kutoa huduma za kijamii (One Stop Service Centre).

5 thoughts on “Serikali Kuanza Utekelezaji wa Mradi Mkubwa wa Uwekezaji Dar es salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama