Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Itaendelea Kuweka Mazingira Bora ya Kuwezesha Vijana Kufanya Biashara na Ujasiriamali

Na Eliud Rwechungura


Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo ameeleza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya kuwezesha vijana kufanya biashara na ujasiriamali ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutengeneza ajira kwa vijana.

Waziri Prof. Mkumbo aliyasema hayo Julai 18, 2021 katika maonesho maalum ya Harusi (Adorable Wedding Trade Fair) yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam yenye dhima ya kukuza tasnia ya harusi nchini Tanzania na kuwajengea uwezo watoa huduma wanaochipukia kufikia viwango vya kimataifa.

“Moja ya majukumu ambayo tumekabidhiwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kutengeneza ajira kwa vijana, Serikali haina uwezo wa kuwaajiri wahitimu wote, ila njia ya kuajiri vijana wengi ni kutengeneza mazingira ili vijana wafanye ujasiriamali, wafanye biashara kubwa na ndogo ndogo”, ameeleza Prof. Kitila Mkumbo.

One thought on “Serikali Itaendelea Kuweka Mazingira Bora ya Kuwezesha Vijana Kufanya Biashara na Ujasiriamali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama