Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Inatambua Mchango Uliotolewa na Balozi Rupia – Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inatambua mchango mkubwa uliotolewa na marehemu Balozi Paul Rupia wakati wa utumishi wake na hata baada ya kustaafu.

“Moja ya jambo ambalo halitasahaulika ni uthubutu wake wa kuanzisha Benki ya Watu wa Dar es Salaam (DCB) ambayo alikuwa Mwenyekiti wake na hadi  anaondoka katika uongozi aliicha benki hiyo ikiwa na matawi manane na moja kati ya hayo likiwa jijini Dodoma.”

Mheshimiwa Majaliwa amesema hayo leo Ijumaa (Septemba 23, 2022) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuuaga mwili wa marehemu Balozi Paul Rupia katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama