Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Imezingatia Haki za Binadamu Wakazi wa Ngorongoro Wanaohamia Handeni

Waziri Ndumbaro amesema imekuwa ni muhimu wadau wa Haki za Binadamu kukutana na kujadili suala la Ngorongoro na Loliondo ili kuhakikisha haki za binadamu zinazingatiwa na kujibu hoja zisizo za kweli zinazosambaa kwa haraka katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Awali, Dkt. Ndumbaro alitoa wasilisho katika kikao na Mabalozi kutoka nchi mbalimbali na taasisi za kimataifa, liloonesha jinsi Serikali inavyozingatia haki na malengo yake kuboresha hali ya watanzania wa maeneo ya Ngorongoro na Loliondo.

Waziri Ndumbaro alisema kwa upande wa Loliondo, Serikali imewapa wananchi zaidi ya asilimia 62 ya eneo la hifadhi ya Loliondo ili kukidhi mahitaji ya wakazi wa sasa na imebakiwa na kiasi cha Kilomita za mraba 1500 kutoka 4000 za awali.

Mawasilisho ya wataalam yameonesha umuhimu wa kuhifadhi maeneo ya Loliondo na Ngorongoro kutokana na sababu za kimazingira na Ikolojia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama