Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Serikali Imezingatia Haki za Binadamu Wakazi wa Ngorongoro Wanaohamia Handeni

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza katika kikao na wadau wa Haki za Binadamu pamoja na Wakuu wa Mikoa ya Arusha na Tanga, Mhe. John Mongella na Mhe. Adam Malima. kikao hiki kimefanyika leo jijini Arusha

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali imezingatia vyema suala la Haki za Binadamu kwa wakazi waliokuwa wanaishi Ngorongoro kisha kuamua kuanza kuondoka kwa hiyari yao kuelekea Kijiji Cha Msomera wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.

Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo leo Juni 21, 2022 kwenye kikao na wadau wa Haki za Binadamu pamoja na Wakuu wa Mikoa ya Arusha na Tanga, Mhe. John Mongella na Mhe. Adam Malima.

“Serikali imezingatia vyema haki za binadamu, imewajengea nyumba wananchi walioamua kuhama kwa hiyari yao, imewapa maeneo yasiyopungua hekari 3 kila mmoja, imewasafirisha wao na mizigo yao na mifugo wanayomiliki, lakini pia Serikali imewalipa fidia”, ameeleza Dkt. Ndumbaro.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama