Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

SADC Yatoa Dola Milioni 6 Ujenzi wa Reli ya Kimataifa ya Mtwara -Mbambabay

Na. Beatrice Sanga-Maelezo

Jumuiya ya kiuchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wametoa Dola za Kimarekani milioni 6 kwa ajili ya kufanyika upembuzi yakinifu wa ujenzi wa reli ya kimataifa ya Mtwara mpaka Mbambabay ambayo inategemewa kufungua fursa nyingi kwa wananchi wa Mtwara na kanda ya Kusini

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari katika kikao cha mkutano wa SADC ambao unahusisha mawaziri wa fedha na uwekezaji wa nchi wanachama wa jumuiya ya SADC uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Akieleza mambo ambayo yanaendelea kujadiliwa na mafanikio ambayo yamefikiwa kutokana na kikao hicho Waziri jamal Kassim ali amesema kikao hicho kimepata fursa ya kujadili mambo mbalimbali yanayohusu sera ya kifedha , za kikodi pamoja na uwekezaji na biashara katika Kanda ya Jumuiya ya SADC ambapo pamoja na hayo fedha zilizotolewa na SADC zinaenda kusaidia upembuzi yakinifu wa ujenzi wa reli hiyo ya Mtwara-Mbambabay ambayo itaenda kufungua uchumi wa Mtwara na kanda nzima ya kusini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama