Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

RC Mongella: Watendaji Serikalini Waelimishwe Kutoa Haki kwa Wakati

Mwenyekiti wa THBUB, Jaji (Mst.) Mathew Mwaimu (katikati) akiongea wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) ofisi kwake jijini Mwanza Aprili 20, 2020. Kushoto ni Kaimu Katibu Mtendaji wa THBUB, Hajjat Fatma Muya.

Na Mbaraka Kambona

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella ameishauri Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) kuandaa mpango maalum wa kutoa elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora  kwa watendaji wa ngazi za mikoa ili waweze kutoa haki za  wananchi kwa wakati.

Mongella alitoa rai hiyo katika kikao kifupi kilichofanyika baina yake na Mwenyekiti wa THBUB, Jaji (Mst.) Mathew Mwaimu alipomtembelea  ofisini kwake  jijini Mwanza Aprili 20, 2020.

Akiongea katika kikao hicho Mongella alisema kuwa kuna haja ya Tume kuweka utaratibu wa kutoa elimu kwa viongozi wa ngazi za mikoa kupitia vikao vyao vya kiutendaji ili kuwajengea uwezo kuhusu masuala ya haki za binadamu na utawala bora na kujua  wajibu wao.

Afisa Mfawidhi wa Ofisi za THBUB Kanda ya Ziwa, Albert Kakengi (kushoto) akimuonesha Kaimu Katibu Mtendaji wa THBUB, Hajjat Fatuma Muya (Kulia) baadhi ya machapisho kuhusu haki za watoto yaliyopo katika maktaba ndogo ofisini hapo. Wa pili kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo Mipango wa THBUB, Laurent Burilo. Uongozi wa THBUB ulitembelea Ofisi hizo za Mwanza Aprili 20, 2020.

“Ni vizuri mkaweka utaratibu kupitia vikao vya Watendaji Wakuu katika mikoa ili kuwaelimisha juu ya dhana nzima ya utoaji haki kwa wananchi, ni muhimu kuwaelimisha viongozi hawa kujua haki na wajibu wao, kwani  bila kufanya hivyo matatizo hayo ya kutopata ushirikiano kutoka kwao yataendelea kuwa changamoto kwenu”, alisema Mongella.

Aliongeza kuwa taasisi za serikali hazina budi kufanya kazi kwa pamoja kwa sababu lengo lao ni kuhudumia wananchi, hivyo ni muhimu kupitia vikao hivyo vya watendaji Tume ikavitumia kuwaelimisha pia kujenga uhusiano utakao warahisishia utendaji kazi wake.

 “Kuna wakati haki inachelewa kushughulikiwa na viongozi aidha kwa sababu ya uzembe au kwa kiongozi  kutokujua wajibu wake katika kutoa haki hiyo ya mwananchi kwa wakati”, aliongeza Mongella

“Tunaweza tukawa tunapambana na matokeo wakati kabla ya matokeo kuna chanzo. Tutoe elimu kwa viongozi, tukiweza kuwaelimisha vizuri naamini tutapunguza kushughulika na matokeo na malalamiko yatapungua”, alisisitiza

Akiongea mapema, Jaji Mwaimu alimueleza Mkuu wa Mkoa huyo kuwa nia ya Tume ni kuisaidia na kuijenga zaidi Serikali ili iweze kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi kwa kuzingatia haki za binadamu na utwala bora na njia pekee ya kufanya hivyo ni kwa Tume kushirikiana kwa karibu na taasisi nyingine za Serikali ambazo zinatoa huduma kwa wananchi.

Jaji Mwaimu aliendelea kusema kuwa ni vigumu kuhamasisha masuala ya haki za binadamu bila kuwahusisha wadau ambao kwa kiasi kikubwa ni Serikali.

Jaji Mwaimu alikutana na Mongella ikiwa ni sehemu ya ziara yake jijini Mwanza ambayo lengo lake kubwa ni kutembelea ofisi za Tume zilizopo kanda ya ziwa ili kushughulikia malalamiko ya wananchi yaliyowasilishwa  katika ofisi hizo.

4 thoughts on “RC Mongella: Watendaji Serikalini Waelimishwe Kutoa Haki kwa Wakati

 • August 10, 2020 at 12:08 pm
  Permalink

  Hi there, its pleasant article concerning media print, we all be
  familiar with media is a impressive source of information.

  Reply
 • August 11, 2020 at 7:32 am
  Permalink

  My spouse and I stumbled over here different web address and thought I should check things out.

  I like what I see so now i am following you. Look forward to exploring your web page yet again. adreamoftrains web host

  Reply
 • August 25, 2020 at 8:03 pm
  Permalink

  I really like your blog.. very nice colors
  & theme. Did you make this website yourself or did
  you hire someone to do it for you? Plz respond as I’m looking to construct my own blog and would like to find out where
  u got this from. cheers 3aN8IMa cheap flights

  Reply
 • October 22, 2020 at 7:49 pm
  Permalink

  your vandal roughly what foundation may be halfway pro you. tadalafil Enrollment’s Schoolyard and the DPS Right hand UN miscellaneous

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama