Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais wa Zanzibar Dk. Shein Ahudhuria Mazishi ya Mama Yake Meja Staaf Juma Kassim Tindwa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakishiriki katika Sala ya kuuombea dua Mwili wa Marehemu Mtumwa Mgeni , mama mzazi wa Meja Mstaaf na Mshauri wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Juma Kassim Tindwa, sala hiyo imefanyika katika msikili wa Kilimani na kuzikwa katika makaburi ya Kwarara.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiika mcha katika kaburi la marehemu Mtumwa Mgeni Mama Meja Mstaaf Juma Kassim Tindwa, mazishi hayo yemefanyika katika makaburi ya Kwarara Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiitikia dua inayosomwa na Sheikh Sharif Abdulrahaman Sharif, wakatika wa mazishi ya Marehemu Mtumwa Mgeni yaliofanyika katika makaburi ya Kwarara Zanzibar.

66 thoughts on “Rais wa Zanzibar Dk. Shein Ahudhuria Mazishi ya Mama Yake Meja Staaf Juma Kassim Tindwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *