Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais wa DRC Atembelea Bandari ya Dar Es Salaam, Akagua Maendeleo ya Ujenzi wa SGR

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akipewa maelezo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isaack Kamwelwe kuhusu maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na njia itamopita wakati mgeni huyo alipotembelea sehemu ya mradi huo eneo la Vingunguti ‘Mahakama ya Mbuzi’ jijini Dar es Salaam leo Juni 14, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa kongo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akitambulishwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isaack Kamwelwe kwa Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli Tanzania, Masanja Kadogosa alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR na njia itamopita wakati alipotembelea sehemu ya mradi huo eneo la Vingunguti ‘Mahakama ya Mbuzi’ jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019

 

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo (DRC) Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akioneshwa mataluma ya reli na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isaack Kamwelwe kwa viongozi wa kampuni ya upakuaji Makontena ya Tanzania International Containers Terminal Services (TICTS) alipotembelea Bandari ya Dar es salaam jijini Dar es salaam leo Juni 14, 2019.

 

135 thoughts on “Rais wa DRC Atembelea Bandari ya Dar Es Salaam, Akagua Maendeleo ya Ujenzi wa SGR

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama