Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Samia Kuwezesha Usafiri wa Wajasiriamali Wadogo Kushiriki Maonesho ya Jua kali Uganda – Waziri Ndalichako

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan atawezesha usafiri wa Wajasiriamali Wadogo na wa Kati 250 kushiriki maonesho ya 22 ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu kama Nguvu Kazi au Jua Kali yatakayofanyika Jijini Kampala, Uganda kuanzia tarehe 8 hadi 18 mwezi Desemba, 2022.

“’Kipindi cha miaka mingi, pamoja na mambo mengine, Serikali imekuwa ikichangia usafiri wa mizigo ya Wajasiriamali kwenda kwenye maonesho. kwa mwaka huu, Serikali yetu inayoongozwa na Mhe. Rais Samia imepanga kuongeza mchango wake kwa kuwezesha usafiri wa basi la wajasiriamali kwenda na kurudi Uganda“

Mhe. Ndalichako amefafanua kuwa, Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu itatumia maonesho hayo kwa lengo la kuwawezesha vijana wajasiriamali wa Tanzania kutumia fursa hiyo kutafuta masoko katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na  kuwawezesha vijana kujiajiri na hivyo kukuza ajira na kuondoa umaskini.

6 thoughts on “Rais Samia Kuwezesha Usafiri wa Wajasiriamali Wadogo Kushiriki Maonesho ya Jua kali Uganda – Waziri Ndalichako

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama