Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Samia Atuma Salamu za Pole Kufuatia Kifo cha Mama Anna Mgwira

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira kilichotokea leo tarehe 22 Julai, 2021 katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru mkoani Arusha alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mhe. Rais Samia amesema amepokea taarifa za kifo cha Mhe. Anna Mghwira kwa majonzi na masikitiko makubwa hasa akikumbuka mchango wake mkubwa alioutoa katika ujenzi wa taifa.

Amewaomba wanafamilia wote wawe na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amemuombea marehemu Anna Mghwira apumzike mahali pema peponi, Amina.

Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

10 thoughts on “Rais Samia Atuma Salamu za Pole Kufuatia Kifo cha Mama Anna Mgwira

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama