Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Samia Atoa Bilioni 500 Ununuzi wa Vifaa vya Kuhudumia Mizigo Bandari ya Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Erick Hamisi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wadau wa bandari kilichofanyika leo Jijini Tanga

Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu imetoa Shilingi bilioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kuhudumia mizigo ili kuongeza ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Erick Hamisi wakati wa mkutano wa wadau wa bandari unaofanyika Jijini Tanga ambapo alisema uwekezaji huo unaokwenda kufanyika katika bandari hiyo ni mkubwa ambao utafungua fursa kwa nchi na maziwa makuu kwa matumizi ya bandari hiyo.

Alisema kuwa kuna mradi wa ujenzi wa bandari kavu ya Kwara ambapo watapeleka mizigo ya nje katika nchi za Maziwa Makuu (Transit) baada ya Serikali kuwekeza fedha hizo ambazo pia zitatumika kununulia vifaa ili kuwezesha ufanisi huo.

4 thoughts on “Rais Samia Atoa Bilioni 500 Ununuzi wa Vifaa vya Kuhudumia Mizigo Bandari ya Dar es Salaam

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama