Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Mstaafu Mhe. Benjamin William Mkapa Awasili Chato kwa Ajili ya Kukabidhi Nyumba 50 za Watumishi wa Afya Katika Mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa alipowasili Chato mkoani Geita. Rais Mstaafu kesho anatarajia kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa sekta ya Afya zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa katika mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida mara baada ya kuwasili Chato mkoani Geita. Balozi huyo wa Japan kesho anatarajiwa kukabidhi mtambo wa kukamua Mafuta ya Alizeti (Double Refine) uliojengwa Chato mkoani Geita kwa Msaada wa Serikali ya Japan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa pamoja na wageni mbalimbali waliofika Chato kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazotarajiwa kufanyika kesho.

(Picha Zote na Ikulu)

73 thoughts on “Rais Mstaafu Mhe. Benjamin William Mkapa Awasili Chato kwa Ajili ya Kukabidhi Nyumba 50 za Watumishi wa Afya Katika Mikoa ya Simiyu, Kagera na Geita

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *