Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Mhe. Dkt. Magufuli Akutana na Rais wa Zambia Edgar Lungu, Tunduma Mkoani Songwe Kufungua Kituo cha Pamoja cha Forodha

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kuwasili Tunduma mkoani Songwe kwa ajili ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu wakati wakipita kwenye Gadi ya Heshma iliyoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika eneo hilo la Tunduma mkoani Songwe.

Wafanyakazi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania na Zambia wakiwa tayari kwa kutoa huduma katika eneo hilo la mpakani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu wakati wakisalimia wananchi mara baada ya kuwasili katika Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu akifurahia hotuba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu kabla ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya ufunguzi wa Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kufungua Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Nakonde Zambia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda mti pamoja na Rais wa Zambia Mheshimiwa Edgar Chagwa Lungu mara baada ya kufungua Kituo cha pamoja cha Huduma za Mpakani (One Stop Border Post) upande wa Nakonde Zambia . (Picha na Ikulu)

 

193 thoughts on “Rais Mhe. Dkt. Magufuli Akutana na Rais wa Zambia Edgar Lungu, Tunduma Mkoani Songwe Kufungua Kituo cha Pamoja cha Forodha

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama