Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

RAIS MAGUFULI: Tuimarishe Umoja na Mshikamano Kuijenga SADC Kuleta Maendeleo kwa Wananchi

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika(SADC) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.Paramagamba Kabudi wakisaini Moja ya Mikataba iliyosainiwa wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika Jijini Dar es Salaam,Tanzania.

Wakuu wa Nchi na Seriakali za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) wakisaini mikataba ya makubaliano katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Wafalme uliofanyika Jijini Dar es Salaam, Tanzania

Na Mwandishi Wetu, MAELEZO 

RAIS Dkt. John Magufuli amewataka Wakuu Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuendelea kuimarisha Umoja na Mshikamano na kuwa na sauti moja katika kusimamia maslahi mapana ya Jumuiya hiyo katika kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

Akifunga Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya hiyo, leo Jumapili (Agosti 18, 2019), Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo alisema Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano unaohitaji ili kuharakisha jitihada za kuleta maendeleo katika jumuiya hiyo.

Aliongeza kuwa Umoja ni kiungo muhimu cha maendeleo katika ushirikiano wa Jumuiya yoyote, hivyo ili kuleta kasi ya mabadiliko ndani ya Jumuiya hiyo ni wajibu wa Nchi wanachama kuhakikisha inatumia vyema rasilimali zake pamoja na kuweka mkazo wa maazimio na agenda za Mkutano wa 39 kwa kutafakari masuala muhimu ya maendeleo.

Rais Magufuli alisema chini ya Uongozi wake, jumuiya hiyo itaendelea kusimama imara na kuwa na nguvu ya pamoja katika kutetea maslahi ya Nchi wanachama ikiwemo vikwazo ilivyowekewa Nchi ya Zimbabwe na kusema Viongozi wa Jumuiya hiyo kwa kauli moja wameungana katika kuitaka jumuiya ya kimataifa kuondoa vikwazo dhidi ya nchi hiyo.

Mwenyekiti wa Ogani ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC,Emmerson Mnangagwa ambaye pia ni Rais wa Zimbabwe akisaini Mkataba kati ya mikataba minne ya itifaki aliyoisaini wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika Jijini Dar es Salaam,Tanzania.

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika(SADC), Dkt.Stagomena Tax na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Botswana, Jan Sadek, Wakisaini Mikataba ya Programu za Maendeleo ya Viwanda SADC, Uwezeshaji wa Biashara na Michakato ya Uimarishaji Viwanda Nchi za SADC, kazi hiyo ilifanyika wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Jumuiya hiyo uliofanyika Jijini Dar es Salaam,Tanzania.

“Tutahakikisha kuwa jumuiya yetu inaondoa changamoto mbalimbali zinazozuia ukuaji wa uchumi ukiwemo vitendo vya rushwa na ukiritimba vinavyokwamisha sekta ya sekta ya biashara baina ya nchi zetu” alisema Rais Magufuli.

Akifafanua zaidi, Rais Magufuli alisema katika mkutano huo wa 39, Wakuu wa Jumuiya hiyo kwa pamoja wameweza kuwa na mjadala wa pamoja uliowawezesha Viongozi hao kutoa maoni, ushauri na michango yao na pamoja kusaini itifaki mbalimbali zilizoridhia agenda na mikakati mbalimbali kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya Jumuiya hiyo.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema kutokana na kasi ndogo ya ukuaji uchumi iliyopo kwa sasa ndani ya jumuiya hiyo, aliwataka Viongozi hao kuhakikisha wanaweka mkazo katika kukuza na kuimarisha sekta ya miundombinu pamoja na kuboresha sera za kifedha na kiuchumi ili kukuza kiwango cha ukuaji wa Pato la Taifa kwa kila Nchi mwanachama.

Rais Magufuli pia aliitaka Sekretarieti ya Jumuiya kutumia fedha kwa malengo yaliyokusudiwa badala ya fedha hizo kutumika katika kuandaa makongamano, warsha na semina mbalimbali na sasa zielekezwe katika utekelezaji wa miradi inayoweza kuleta manufaa kwa nchi wanachama ndani ya jumuiya hiyo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wakifurahia jambo katika Mkutano Mkuu wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) uliofanyika Jijini Dar es Salaam,Tanzania.

“Tutahakikisha kuwa jumuiya yetu inaondoa changamoto mbalimbali zinazozuia ukuaji wa uchumi ukiwemo vitendo vya rushwa na ukiritimba vinavyokwamisha sekta ya sekta ya biashara baina ya nchi zetu” alisema Rais Magufuli.

Akifafanua zaidi, Rais Magufuli alisema katika mkutano huo wa 39, Wakuu wa Jumuiya hiyo kwa pamoja wameweza kuwa na mjadala wa pamoja uliowawezesha Viongozi hao kutoa maoni, ushauri na michango yao na pamoja kusaini itifaki mbalimbali zilizoridhia agenda na mikakati mbalimbali kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya Jumuiya hiyo.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli alisema kutokana na kasi ndogo ya ukuaji uchumi iliyopo kwa sasa ndani ya jumuiya hiyo, aliwataka Viongozi hao kuhakikisha wanaweka mkazo katika kukuza na kuimarisha sekta ya miundombinu pamoja na kuboresha sera za kifedha na kiuchumi ili kukuza kiwango cha ukuaji wa Pato la Taifa kwa kila Nchi mwanachama.

Rais Magufuli pia aliitaka Sekretarieti ya Jumuiya kutumia fedha kwa malengo yaliyokusudiwa badala ya fedha hizo kutumika katika kuandaa makongamano, warsha na semina mbalimbali na sasa zielekezwe katika utekelezaji wa miradi inayoweza kuleta manufaa kwa nchi wanachama ndani ya jumuiya hiyo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika(SADC) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, akihutubia wakati wa kufunga Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC uliofanyioka Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Aksoni akiteta jambo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Kathe Kamba, kabla ya Sherehe za Kufunga Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za SADC uliofanyioka Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

“Katika Bajeti yetu ya mwaka 2019/2020 tumepanga kutumia Dola Milioni 74, mchango wa Dola Milioni 43 zinazotolewa nan chi wahisani tunaweza kujenga vituo 17, nitafurahi kuona siku moja Sekretarieti ya jumuiya yetu ikiwaalika wanachama katika uzinduzi wa vituo hivyo” alisema Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli aliwakaribisha wawekazaji waliopo ndani ya SADC kuja kuwekeza katika miradi ya sekta mbalimbali iliyopo nchini ikiwemo nishati, madini, utalii, mifugo, kilimo pamoja na utalii kwani Tanzania imeweka mazingira bora na wezeshi kwa kwa ajili ya wawekezaji na wafanyabiashara.

Akizungumzia kuhusu maombi ya Nchi ya Burundi kujiunga na Jumuiya hiyo, Rais Magufulli alisema Sekretarieti ya jumuiya hiyo imepanga kutuma timu ya uchunguzi katika nchi hiyo kwa ajili ya kujiridhisha na masuala muhimu ya kimsingi yanayopaswa kuzingatiwa kabla ya kukubaliwa kwake kujiunga na Jumuya hiyo.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Dkt.Bashiru Ally akisalimiana na Mawaziri Wakuu Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Malecela(kulia) na Mizengo Pinda (Kushoto), kabla ya Sherehe za Kufunga Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi za SADC uliofanyioka Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo, Dkt. Stegomena Tax alisema Mkutano huo wa 39 wa SADC umekuwa wa mafanikio makubwa kutokana na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Nchi wanachama ambapo wameweza kuweka mikakati ya pamoja itakayosaidia kuongeza kasi ya ukuaji uchumi na maendeleo ya Nchi hizo.

Dkt. Tax alisema kuwa katika mkutano huo pia, Viongozi wa Jumuiya hiyo waliweza kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi wa ndani katika Jumuiya hiyo ikiwemo Nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ndani ya Jumuiya hiyo (TROIKA) aliyokwenda kwa Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa.

90 thoughts on “RAIS MAGUFULI: Tuimarishe Umoja na Mshikamano Kuijenga SADC Kuleta Maendeleo kwa Wananchi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama