Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Dkt. Magufuli Awaasa Watanzania Kulinda Amani, Umoja na Mshikamano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza wananchi kutunza amani na utulivu hapa nchini wakati wa maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru na miaka 57 ya Jamhuri yaliyofanyika Jijini Mwanza leo Desemba 9, 2019.

Na Mwandishi wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka Watanzania kudumisha amani na mshikamano uliopo ili kuimarisha msingi wa maendeleo ya Taifa.

Akizungumza  wakati wa maadhinmisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miaka 57 ya Jamhuri, leo (Jumatatu Desemba 9, 2019) Rais Magufuli amesema kuwa mafanikio yaliyofikiwa tangu uhuru yanatokana na juhudi zilizochukuliwa na viongozi wa Awamu ya kwanza hadi sasa zikilenga kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimu wananchi waliojitookeza kushiriki maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru na miaka 57 ya Jamhuri yaliyofanyika Jijini Mwanza leo Desemba 9, 2019.

“Serikali ya Awamu ya Awamu ya Tano imejipanga kulinda uhuru wetu, umoja wetu, muungano wetu, na kulinda mafanikio yaliyofikiwa katika kipindi cha mika 58 ya uhuru” alisisitiza Rais Dkt. MagufuliAkizungumzia mafanikio ya miaka 58 ya uhuru amesema kuwa wakati taifa linapata uhuru mwaka 1961 kulikuwa na kilomita 360 za barabara zenye lami wakati kwa sasa barabara zenye lami ni zaidi ya elfu 12,000, huku kilometa  2400 zinajengwa, na 7087 zikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride wakati wa maadhimisho ya siku ya miaka 58 ya uhuru wa Tanzania Bara na miaka 57 ya Jamhuri leo Jijini Mwanza

Kwa upande wa sekta ya elimu, Rais Magufuli anasema wakati wa uhuru mwaka 1961 kulikuwa na chuo kikuu kimoja wakati kwa sasa viko vyuo vikuu 48, hali inayodhibitisha kukua kwa kiwango cha elimu na kuchochea ustawi wa wananchi.

Kwa upande wa sekta ya viwanda amesema kuwa hadi sasa kuna takribani viwanda 4000 vilivyojengwa katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Tano ikiwa ni sehemu ya Serikali kuimarisha na kukuza sekta hiyo kama ilivyokuwa wakati wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Komando wa Kikosi cha Komando kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakionesha onesho lao wakati wa maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru na miaka 57 ya Jamhuri leo Desemba 9,2019 Jijini Mwanza.

Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imeweka mkazo katika kuboresha huduma za jamii kama maji,nishati, miundombinu, viwanda, elimu, afya na ukuzaji wa kilimo ili kuchochea  ukuaji wa viwanda.

Katika sekta ya uchukuzi Dkt. Magufuli amesema Serikali inaendelea na ujenzi na upanuzi wa viwanja 11 na ununuzi wa ndege 11 ili kuimarisha sekta ya uchukuzi nchini.

Askari wa Majeshi ya ulinzi na usalama wakipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru na miaka 57 ya Jamhuri yaliyofanyika Jijini Mwanza Desemba 9, 2019.

Katika hatua nyingine Rais Dkt.  Magufuli ametoa msamaha kwa wafungwa 5,535 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanzania bara na kuwaasa watakaonufaika na msamaha huo kuacha kutenda makosa kwa mara nyingine kwa kuwa raia wema.

Maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru na miaka 57 ya Jamhuri yamefanyika Disemba 9, 2019 Jijini Mwanza na kupambwa na gwaride la vikosi vya ulinzi na usalama, kwaya, ngoma na onesho kutoka kwa kikosi cha Komando.

228 thoughts on “Rais Dkt. Magufuli Awaasa Watanzania Kulinda Amani, Umoja na Mshikamano

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama