Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Magufuli Atoa Billioni 15 Kumalizia Ujenzi Hospitali ya Mwalimu Nyerere Mara

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu(kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima wakati walipokutana mkoani Marawakati Mawaziri hao walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo mkoani Mara.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa kiasi cha shillingi Billioni 15 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyojengwa kwa miaka 40 bila kumalizika.

Haya yamebainika wakati wa ziara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu  na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi katika hospitali hiyo kujionea maendeleo ya ujenzi wake.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu(kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima wakati walipokutana mkoani Mara wakati Mawaziri hao walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo mkoani Mara.

Akizungumza mara baada ya kutembelea Hospitali hiyo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Hospitali hiyo itakuwa masaada mkubwa kwa wananchi wa mkoa wa Mara hasa kwa huduma za matibabu ya kibingwa.

“Kutakuwa hakuna haja ya kwenda Hospitali ya Kanda Bugando kupata matibabu ya kibingwa kwani tunataka huduma za kibingwa zitolewe hapa hapa”alisema

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amesema kuwa Shirika la Nyumba na Chuo Kikuu cha Ardhi kimepewa kazi ya kusimamia ujenzi wa Hospitali hiyo hivyo ameagiza kazi kufanyika usiku na mchana ili limalizike kwa muda uliopangwa.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima wakikagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo mkoani Mara.

“Tumekubaliana tarehe 17 mwezi huu wa tatu wawe wamekamilisha Wing C ili huduma za Mama na mtoto zinanze kutolewa kwa muda husika” alisema

Kwa upande wake Mkuu Mkoa wa Mara Adam Malima amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha kwa ajili ya kumalizia hospitali hiyo iliyokwama kwa muda wa miaka 40 mpaka sasa.

“Hospitali hii imechukua awamu tano za marais kumalizika na tunamshukuru Rais kwa kuchukulia kipaumbele katika hili” alisema

4 thoughts on “Rais Magufuli Atoa Billioni 15 Kumalizia Ujenzi Hospitali ya Mwalimu Nyerere Mara

 • March 21, 2021 at 9:33 am
  Permalink

  Excellent pieces. Keep writing such kind of information on your page.
  Im really impressed by your site.
  Hi there, You’ve done an incredible job. I will definitely digg
  it and in my view suggest to my friends. I’m sure
  they’ll be benefited from this website.

  Reply
 • March 25, 2021 at 9:46 pm
  Permalink

  Hi there! I know this is kind of off topic but I was wondering
  which blog platform are you using for this site? I’m getting tired of WordPress because I’ve had problems with hackers and I’m looking at options for another platform.

  I would be great if you could point me in the direction of a good platform.

  Reply
 • March 26, 2021 at 1:13 pm
  Permalink

  Hello everyone, it’s my first pay a visit at this web page, and article is genuinely fruitful
  for me, keep up posting these posts.

  Reply
 • March 28, 2021 at 12:05 pm
  Permalink

  Have you ever considered about adding a little bit more than just
  your articles? I mean, what you say is fundamental and everything.

  However just imagine if you added some great pictures or videos to
  give your posts more, “pop”! Your content is excellent
  but with images and clips, this website could undeniably be one of the greatest in its niche.
  Good blog!

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama