Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Magufuli Atoa Bilioni 10 Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein
Mwinyi pamoja na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo na maafisa
waandamizi wengine akifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa  jiwe la
Msingi  la ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa(National Defence Headquarters) katika eneo la Kikombo  Jijini Dodoma leo Jumatatu Novemba 25, 2019

Na Jonas Kamaleki- MAELEZO, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa shilingi bilioni 10 ili
ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinziwa Taifa uanze eneo la Kikombo, Wilaya ya Chamwino, Dodoma.
Rais Magufuli amesema kuwa uamuzi wa kujenga Makao Makuu hayo Jijini Dodoma ni jambo la
kizalendo ambalo linatimiza ndoto ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ya
kuhamishia Makao Makuu Dodoma.

“Mwaka 2015 wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 nilitoa ahadi ya kuhamishia Makao Makuu ya
nchi Dodoma ili kutimiza ndoto ya miaka zaidi 40 ya Baba wa Taifa, sasa imetimia na jeshi limehamia
Dodoma,”alisema Rais Magufuli.

Amiri Jeshi Mkuu amesema kuwa Jeshi la Wananchi limesaidia sana kuleta amani na si kwa Tanzania tu
bali Lebanon, Uganda, Jumhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na nchini nyingine nyingi Duniani.

Akiweka jiwe na msingi la ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, Rais aliamuru maandalizi ya ujenzi
ya barabara ya kuelekea eneo hilo yaanze wiki ijayo ili barabara ijengwe kwa kiwango cha lami.

Kuhusu fidia ya waliokuwa wakazi wa eneo ambalo limetwaliwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi huo, Rais
Magufuli amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi kuanza kuwalipa fidia kuanzia
tarehe 1, Desemba, 2019.

Mkazi wa Kijiji cha Kikombo, Paul Andrew amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuagiza walipwe fidia
na kuwajengea barabara kwa kiwango cha lami.

“Kwa kweli tunamshukuru Mhe. Rais kwa uamzi wake wa kutufidia kwani tumekaa miaka miwili bila
kulima kwenye maeneo yetu na bila kulipwa chochote,” alisema Andrew.

Ujenzi huu ni wa kihistoria kwani tangu Uhuru wa Tanganyika, Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa
unajengwa na Serikali ya Tanzania.

31 thoughts on “Rais Magufuli Atoa Bilioni 10 Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama