Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Magufuli amemteua Brig. Jen Dkt. Mhidize kuwa Mkurugenzi Mkuu MSD

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Brig. Jen Dkt. Gabriel Sauli Mhidize kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (Medical Stores Department – MSD).

Uteuzi wa Brig. Jen Dkt. Mhidize unaanza mara moja, leo tarehe 03 Mei, 2020.

Kabla ya uteuzi huo, Brig. Jen Dkt. Mhidize alikuwa Mkuu wa Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Brig. Jen Dkt. Mhidize anachukua nafasi ya Bw. Laurean Rugambwa Bwanakunu ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Chato

03 Mei, 2020

One thought on “Rais Magufuli amemteua Brig. Jen Dkt. Mhidize kuwa Mkurugenzi Mkuu MSD

  • June 1, 2021 at 10:59 pm
    Permalink

    740825 628151I discovered your web site web site online and check a lot of of your early posts. Keep on the top notch operate. I just now additional your Feed to my MSN News Reader. Looking for forward to reading much far more from you finding out later on! 630394

    Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama