Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Magufuli Afungua Mkutano wa Mashauriano wa Mwaka wa Wadau Mbalimbali wa Sekta ya Ujenzi Nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wadau mbalimbali kutoka Bodi ya Usajili Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Bodi ya Usajili Wakandarasi (CRB) Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) pamoja na wadau wa Sekta ya Ujenzi kabla ya kufungua mkutano huo wa Mwaka wa Mashauriano katika Bodi na Taasisi hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mchungaji Daniel Mgogo mara baada ya kufungua mkutano huo wa Mashauriano uliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia vitasa mbalimbali vya Milango wakati alipopita kukagua mabanda katika maonesho ya Wadau wa Sekta ya Ujenzi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Charles Kitwanga Mbunge wa Misungwi mara baada ya kukagua mabanda katika maonesho ya Wadau wa Sekta ya Ujenzi yaliyopo katika viwanja vya Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

 

27 thoughts on “Rais Magufuli Afungua Mkutano wa Mashauriano wa Mwaka wa Wadau Mbalimbali wa Sekta ya Ujenzi Nchini

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *