Karibuni kwenye Blogu Rasmi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu ni Uwanja wa Wananchi Kupata Taarifa Mbalimbali za Serikali na Masuala Mengine ya Kijamii, Kisiasa, na Kiuchumi. Blogu hii inaratibiwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali kupitia Idara ya Habari (MAELEZO).

Rais Magufuli Aagiza Maafisa TANROADS Kusimamishwa Kazi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akiwasili eneo la daraja la Kiegeya lililosombwa na maji na kukata
mawasiliano barabara ya Dodoma-Morogoro akiwa ameongozana na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Aloyce Mamwelwe, Mkuu wa Mkoa
wa Morogoro Mhe. Loatha Sanare na viongozi wengine wa Wizara na mkoa
huo leo Jumatatu Machi 16, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli akitembelea maeneo mbalimbali yaliyozunguka daraja la Kiegeya
lililosombwa na maji na kukata mawasiliano barabara ya Dodoma-Morogoro
akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Aloyce Mamwelwe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loatha Sanare
na viongozi wengine wa Wizara na mkoa huo leo Jumatatu Machi 16, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa aliyekuwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) katika Mkoa wa Morogoro Mhandisi Godwin Andalwisye na wahandisi wake 12 waliokuwa na jukumu la uangalizi wa barabara katika Mkoa huo.

Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 16 Machi, 2020 baada ya kutembelea eneo la daraja la Kiegeya lililosombwa na maji ya mvua tarehe 02 Machi, 2020 na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara ya Dodoma – Morogoro ambayo ni kiunganishi muhimu cha Mikoa ya Kanda ya Kati, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kaskazini Magharibi na nchi jirani za Uganda, Rwanda, Burundi na DRC ambazo husafirisha mizigo na abiria kwenda Dar es Salaam.

Mawasiliano ya barabara hiyo yalirejea baada ya siku 2 na mpaka sasa eneo hilo linapitika kwa madaraja ya muda huku kazi ya kuimarisha ikiendelea.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli akitembelea maeneo mbalimbali yaliyozunguka daraja la Kiegeya
lililosombwa na maji na kukata mawasiliano barabara ya Dodoma-Morogoro
akiwa ameongozana na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Aloyce Mamwelwe, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loatha Sanare
na viongozi wengine wa Wizara na mkoa huo leo Jumatatu Machi 16, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli akitoa maagizo baada ya kutembelea na kujionea athari
zilizolipata daraja la Kiegeya lililosombwa na maji na kukata
mawasiliano barabara ya Dodoma-Morogoro akiwa ameongozana na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Aloyce Mamwelwe, Mkuu wa Mkoa
wa Morogoro Mhe. Loatha Sanare na viongozi wengine wa Wizara na mkoa
huo leo Jumatatu Machi 16, 2020

Mhe. Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi kwa Maafisa hao wa TANROADS pamoja na kuwachunguza kama kuna vitendo vya hujuma walivifanya, kutokana na kutochukua tahadhari za kitaalamu za kuzuia maji ya mvua yasisombe daraja lililokuwepo na pia kushindwa kurejesha mawasiliano ya barabara kwa kujenga daraja haraka licha ya fedha za kufanyia kazi hizo kuwepo.

Katika mahojiano na Mkurugenzi wa Matengenezo wa TANROADS Mhandisi Mohamed Ntunda, Mhe. Rais Magufuli ameelezwa kuwa hadi daraja la Kiengeya linasombwa na maji ya mvua, TANROADS katika Mkoa wa Morogoro walikuwa na zaidi ya shilingi Bilioni 3 za matengenezo ya dharura ya barabara.

Akiwa katika eneo hilo Mhe. Rais Magufuli ameliona daraja la muda lililojengwa na Wataalamu wa TANROADS na pia ametembea kwa miguu kuelekea mto unakotirisha maji yake ambapo ameshauri wataalamu hao waangalie uwezekano wa kujenga daraja katika eneo jingine lenye umbali mfupi wa daraja na miinuko inayofaa endapo wataona inafaa kufanya hivyo.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemuonya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Aloyce Kamwelwe, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale na Mkurugenzi wa Matengenezo wa TANROADS Mhandisi Mohamed Ntunda kutokana na kutoridhishwa na juhudi zilizofanywa kurejesha mawasiliano ya uhakika katika eneo hilo na ametaka kosa hilo lisirudie.

Ametoa siku 7 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na TANROADS kuhakikisha eneo hilo linakuwa na daraja la uhakika la kupita magari kama ilivyokuwa kabla ya daraja kusombwa na maji ili kutoathiri shughuli za kiuchumi na kijamii kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya barabara.

Mhe. Rais Magufuli amewataka Mameneja wa TANROADS wa Mikoa yote hapa nchini kuhakikisha mawasiliano ya barabara kuu katika Mikoa yao hayakatiki vinginevyo meneja husika atavuliwa wadhifa wake.

Wasafiri na wananchi waliokusanyika katika eneo hilo wakati Mhe. Rais Magufuli akikagua eneo hilo wamelalamikia kukatika kwa mawasiliano ya barabara ya kuelekea Hospitali ya Misheni ya Berega kutokana na kusombwa kwa daraja, hivyo amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loatha Sanare kuhakikisha Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inajenga daraja hilo ndani ya siku 7 ili wananchi waendelee kupata huduma za matibabu kama kawaida.

Halikadhalika wananchi hao wamelalamikia kutokamilika kwa ujenzi wa chumba cha upasuaji katika Kituo cha Afya Magubike na Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuhakikisha jengo hilo linajengwa ndani ya miezi 2.

Pia, Wananchi hao wamelalamikia kuchangishwa shilingi 20,000 kwa kila kaya kwa ajili ya kujenga jengo la maabara katika shule yao ya Sekondari, lakini fedha hizo hazijulikani zilikokwenda na badala yake wameanza kuchangishwa fedha nyingine shilingi 5,000 kwa kila kaya, na Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro Wilbroad Mutafungwa kufuatilia na kuchukua hatua stahiki. Mhe. Rais Magufuli amechangia shilingi Milioni 5 na ameagiza wananchi wasichangishwe fedha za ujenzi wa maabara hiyo.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Morogoro

16 Machi, 2020

10 thoughts on “Rais Magufuli Aagiza Maafisa TANROADS Kusimamishwa Kazi

 • August 11, 2020 at 2:16 am
  Permalink

  Howdy I am so happy I found your webpage, I really found you by accident, while I was looking on Askjeeve for something
  else, Anyhow I am here now and would just like to say kudos for a fantastic post and a all
  round enjoyable blog (I also love the theme/design), I don’t have time to browse
  it all at the minute but I have saved it and also added your RSS feeds, so when I have time I will be
  back to read a lot more, Please do keep up the excellent b.

  Reply
 • August 14, 2020 at 8:07 am
  Permalink

  I loved as much as you’ll receive carried out right here.
  The sketch is attractive, your authored subject matter stylish.
  nonetheless, you command get got an edginess over that you wish be delivering the following.
  unwell unquestionably come further formerly again since exactly the same nearly very often inside case you shield this increase.

  Reply
 • August 14, 2020 at 2:35 pm
  Permalink

  It’s actually a nice and useful piece of information. I am happy that you just shared this helpful info with us.
  Please keep us informed like this. Thanks for sharing.

  Reply
 • August 24, 2020 at 10:02 pm
  Permalink

  This blog was… how do I say it? Relevant!! Finally I’ve found something which helped
  me. Kudos! 3gqLYTc cheap flights

  Reply
 • August 25, 2020 at 6:26 pm
  Permalink

  Hey there, You’ve done a fantastic job.
  I’ll definitely digg it and personally suggest to my friends.
  I’m confident they will be benefited from this site.

  Reply
 • August 31, 2020 at 4:55 am
  Permalink

  That is really interesting, You’re a very skilled blogger.
  I’ve joined your rss feed and look ahead to in quest of more of
  your fantastic post. Additionally, I’ve shared your website in my social networks

  Reply
 • September 5, 2020 at 12:51 pm
  Permalink

  Hi there, I do think your site might be having internet browser
  compatibility issues. Whenever I take a look at your
  web site in Safari, it looks fine however, if opening in IE, it has some overlapping issues.
  I simply wanted to provide you with a quick heads
  up! Apart from that, great website!

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ev eşyası depolama